Sunday, February 8, 2015

QPR MAJANGA JUU YA MAJANGA, 'MUNGU MTU' WAO NJE MSIMU MZIMA!!!!

Austin katikati akijaribu kuwatoka mabeki wa Southampton jana.
Kifo kimezidi kuinyemelea klabu ya QPR kufuatia nyota tegemeo katika harakati za kujinasua kushuka daraja, Charlie Austin na Richard Dunne, kuripotiwa kuwa watakosa mechi zote zilizosalia msimu huu baada ya kuumia katika mchezo wa jana dhidi ya Southampton.
Austin ndiye kila kitu pale Loftus, akiwa ndiye kinara wa mabao wa timu  kwa mabao 13 mpaka sasa, hata hivyo QPR kwa sasa inaanza mikakati wa kupata mbadala wake.
Dunne alijitonesha katika dakika ya 83 jana.

Matumaini ya timu hiyo kubaki ligi kuu yamezidi kunyongonyeshwa, huku jana ikikubali kichapo cha bao la usiku sana la Saido Mane dakika ya 93, hali inayowafanya kubaki katika ukanda wa kushuka daraja.
Inaripotiwa kuwa kocha wa zamani wa Spurs, Tim Sherwood anatajwa kuchukua mikoba ya kukinoa kikosi hicho, baada ya Harry Redknapp kunyosha mikono mapema wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...