Sunday, February 8, 2015

MAN UNITED CHUPUCHUPU 'IGONGWE' NYUNDO UPTON PARK

Manchester United imeponea chupuchupu kukumbana na kichapo kutoka kwa Wagonga Nyundo wa London, West Ham United, baada ya kiungo Daley Blind kuipatia bao la kusawazisha dakika za mwisho kabisa.
Wenyeji, West walitangaulia kupata bao dakika ya 49 kupitia kwa Cheikhou Kouyate  baada ya kutumia vema uzembe wa mabeki wa United  ambapo aliuchezea mpira alivyotaka na kutumbukia nyavuni.
De Gea alikuwa nyota wa mchezo, akipangua moja ya michezo ya hatari kwenye mchezo huo.
Amebana amechia...mpira uliopigwa na Kouyate (kushoto aliyeanguka chini) ukitinga wavuni huku kipa De Gea akiwa amepotea mabyoya.
Mbali na bao hilo, jahazi laUnited lilionekana bayana kupwaya kwa kipindi kirefu huku asimilia kubwa safu ya kiungo kuonekana kucheza chini ya kiwango. Aidha shukurani zote, zitamwendea kipa wao, David De Gea ambaye alifanya kazi kubwa kuokoa hatari nyingi langoni huku United wakifika aghalabu langoni mwa West Ham.
United ilisawazisha bao hilo dakika ya 92 zikiwa zimebakia dakika mbili katika zile za fidia kupitia kwa Blind. Hata hivyo Man wamepata pigo baada ya beki wao, Luke Shaw kupewa kadi mbili za njano na kutolewa kwa kadi nyekundu.
Blind (wa pili kulia) akiifungia United bao la kusawazisha, dakika mbili kabla ya kipyenga cha mwisho.
Kipa wa WEst Ham akiruka bila mafanikio katika kuokoa shuti la Blind.

NUKUU MUHIMU: Man United haijawahi kupata ushindi katika mechi ilizosawazisha tangu Louis Van Gaal aanze kuifundisha timu hiyo. Pia Man U haijawahi kushinda mchezo wowote kwa kutokea nyuma ikiwa kwenye uwanja wa ugenini tangu Desemba 2013.

Katika mechi nyingine, sare iliendelea kutawala, baada ya Newcastle United na Stoke City kutoshana nguvu ya bao 1-1 huku katika mchezo wa awali, Bunley walitutumua na kuisimamisha West Brom kwa kufungana mabao 2-2.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...