Tuesday, August 12, 2014
MCHEKESHAJI MAARUFU WA MAREKANI AJIUA
Muigizaji na mchekeshaji maaarufu wa Marekani, Robin Williams amejiua.
Mwili wake umekutwa nyumbani kwake California, Marekani Jumatatu Agosti
11, 2014.
Muigizaji huyo alikuwa hajitambui na hakuwa anapumua na hivyo kubainika kuwa alijiua kwa kukosa hewa. Williams alionekana nyumbani kwake mara ya mwisho mida ya nne usiku siku ya Jumapili.
Robin alipelekwa rehab mwezi uliopita kujizuia kunywa pombe. Alikuwa akihangaika kuacha kutumia cocaine na pombe katika miaka ya 80 lakini hakuwahi kunywa kwa miaka 20.
WAPAKISTANI WALIO KAMATWA NA UNGA DAR WATOROKA
Wapakistani wawili, Abdul Ghan Peer Bux na Shahbaz Malk (pichani)
waliokamatwa wakiwa na Watanzania wanaotuhumiwa kwa kukutwa na
madawa ya kulevya wametoroka nchini.
Watuhumiwa hao walikamatwa Februari 21, 2011wakiwa na madawa ya
kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 6.2, Mbezi Beach maeneo
ya Jogoo jijini Dar sa Salaam.Habari za uchunguzi ndani ya Mahakama Kuu zinasema kuwa, Jaji Grace Mwakipesile anayesikiliza kesi hiyo inayotarajiwa kuendelea kusikilizwa kesho Jumatano, ametoa amri ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao.
Kesi hiyo ambayo ilisikilizwa mahakamani hapo Julai 4, mwaka huu ilidaiwa kuwa Wapakistani hao walikamatwa na kikosi kazi cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya kisha kudhaminiwa lakini wametoweka bila kuhudhuria mahakamani hata siku moja.
Imeelezwa kuwa, baada ya watuhumiwa hao
kudhaminiwa na wadhimini wawili, Julai 4, mwaka mahakama iliambiwa kuwa
wadhamini hao wamefariki dunia.
Hata hivyo, jaji anayesikiliza kesi hiyo
aliwaagiza ndugu waliotoa taarifa hiyo kupeleka cheti halisi cha kifo
kesho na watuhumiwa wahudhurie mahakamani hapo.
Watanzania waliokamatwa na Wapakistani hao
waliachiwa huru baada ya kulipa dhamana ya shilingi 10,000,000 ambapo
wadhamini wao ni Raza Hussein Kanji ambaye alipewa stakabadhi namba
3406367 na Nazar Mohamed Nurd alikatiwa yenye namba 3406355.
Februari 21, 2011 polisi chini ya kamanda wao, Godfrey Nzowa
waliwakamata Wapakistani hao wakiwa na Watanzania wawili, William Chonde
na Kambi Zuberi ambao wapo nje kwa dhamana wakituhumiwa kukutwa na
madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 6.2.
Subscribe to:
Posts (Atom)