Tuesday, May 27, 2014

MAPICHA:MWILI WA MSANII RECHO KUSAFIRISHWA KWAO SONGEA KWA MAZISHI


MASTAA wa Bongo Muvi wamemlilia msanii mwenzao, Rachel Haule 'Recho' aliyefariki jana saa mbili usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar baada ya kujifungua ambapo mtoto wake alifariki muda mfupi na baadaye yeye akafariki.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve ‘Nyerere’, mwili wa Rachel utasafirishwa kwenda kwao Songea kwa ajili ya maziko. Habari nyingine za msiba zitatolewa wakati wowote na mtandao huu mara tu zinapopatikana.

Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere akilia kwa uchungu.

Huzuni tele ikiwa imetawala wasanii waliokuwa viwanja ya Leaders.

Bi. Mwenda akilia kwa uchungu.

Mume wa Rachel aitwaye Saguda akiwa na majonzi.

Mwigizaji Johari akiwa na huzuni.

Cathy Rupia akiomboleza.

Steve akizungumza na wanachama wa Bongo Muvi, viwanja vya Leaders.

Bongo Muvi wakijadili cha kufanya.

Wasanii wakipanga utaratibu wa msiba wa mwenzao.

Wasanii wa Bongo Muvi wakiwa Muhimbili baada ya kupata habari za kifo cha mwenzao.


Monday, May 26, 2014

HATIMAYE RACHEL HAULE HATUNAYE TENA DUNIANI




Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam. Habari zilizotua Global na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia. Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki kimeleta mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo. Habari na picha zaidi zitawajia baadae






 

Sunday, May 25, 2014

DIAMOND YUKO NDANI YA TEXAS AKIWA NA WENYEJI WAKE DMK, PHANUEL NA INNOCENT TAYARI KWA MAKAMUZI DALLAS NA HOUSTON


HERMON INTERNATIONAL MINISTRY WAKISHIRIKIANA NA BRANEA SPIRITUAL FAMILY WAMEANDAA IBADA MAALUM YA KUPNADA MBEGU KWAAJILI YA WATOTO


HERMON INTERNATIONAL MINISTRY  WAKISHIRIKIANA NA  BRANEA SPIRITUAL FAMILY wamekuandalia ibada maalum ya kupanda Mbegu  kwaajili ya watoto itakayofanyika 30/05/2014 hadi 31/05/2014 na  ibada maalum ya kupanda mbegu kwa ajili ya watoto na maombi itakayofanyika katika ukumbi wa Prayer House Mkwajuni Kinondoni tarehe 01/06/2014 kuanzia saa 4:00 asubuhi.Watakahubiri ni Mch. DAUDI KAISI na Apostle PAUL KAISI

JINSI YA KUFIKA: Kama unataokea Kariakoo panda magari ya Mwananyamala  shuka Mkwajuni, kama unatokea  Mabaga panda magari ya Msasani  shuka kituo cha Mkwajuni . Mawasiliano yetu
Mch. Kiongozi 0713 160 964 0756 073 691Katibu: 0756 716842

Wednesday, May 21, 2014

DAKTARI: KUAMBIANA AMEJIUA

WAANDISHI WETU
IMEVUJA! Siku chache baada ya kifo cha mwongozaji na mwigizaji wa filamu Bongo, Adam Philip Kuambiana, daktari mkubwa wa mastaa ameibuka na kudai marehemu alijiua mwenyewe.

Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu Adam Kuambiana.

Kwa mujibu wa daktari huyo ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini kutokana na maadili ya taaluma yao kuficha siri ya mgonjwa, siku moja kabla ya kifo (Ijumaa ya Mei 16, mwaka huu), marehemu alimpigia simu na kumwambia amekunywa dawa za malaria aina ya Fansidar lakini pia amekunywa pombe.

Mwili wa Adam ukitolewa Viwanja vya Leaders baada ya kuagwa.

ILIVYOKUWA
Daktari huyo alieleza kuwa, marehemu alimpigia simu kumuomba ushauri juu ya nini cha kufanya na kama kuna madhara yoyote juu ya pombe hizo na dawa alizokunywa.

“Aliniuliza kama kuna madhara yoyote ambayo anaweza kuyapata kwa kuwa alikuwa amekunywa fansidar kwa ajili ya malaria kisha akapata kiu ya bia na kuamua kunywa,” alisema daktari huyo.

Mwili wa marehemu Kuambiana ukiwasili kaburini tayari kwa shughuli za kuusitiri.

AMSHAURI KWENDA HOSPITALI
Akizidi kuzungumzia tukio hilo, daktari alikwenda mbele kwa kusema licha ya msanii huyo kuwa na ‘masikhala’ mara kwa mara, lakini kwa kuwa alimwambia jambo ambalo linahusu uhai wake, alimshauri kwenda hospitali iliyo karibu ili akaonane na daktari kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kutoa sumu kwani kitaalam mtu anapokunywa pombe akiwa amemeza dawa za aina hiyo vyote hugeuka kuwa sumu.


Jeneza lenye mwili wa marehemu Kuambiana likishushwa kaburini.

Alisema kutokana na jinsi alivyozidi kumsimulia hali aliyonayo, aliamini kwamba marehemu alikuwa anamaanisha alichokuwa akikisema hivyo ikabidi amsisitize kuwahi hospitali haraka.

“Nilimwambia awahi hospitalini haraka kwani nilijua fansidar ni kali na si dawa ya kufanyia mchezo. Lakini kesho yake nilipopata taarifa za kifo chake niliumia sana japokuwa nilijua amejiua kwa kuchangaya fansidar na bia maana mchanganyiko wa sumu yake mwilini ni mkali sana,” alisema daktari huyo huku akisisitiza kusitiriwa kwa jina lake.


Msanii wa filamu, Richie Richie akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu Kuambiana.

MAZINGIRA YA KIFO
Kwa mujibu wa mtu ambaye alikuwa karibu na Kuambiana siku ya tukio ambaye naye hakutaka kutajwa jina gazetini, marehemu asingekufa ghafla kama tatizo alilokuwa nalo lingekuwa la vidonda vya tumbo ambavyo vilikuwa vikimsumbua kwa muda mrefu.

“Siku ile marehemu alikuwa na pesa, alikunywa sana pombe kutoka asubuhi mpaka usiku mwingi, alikuwa anakula kila anapojisikia sasa hatuelewi ni kitu gani kilitokea maana haiwezekani mtu akutwe anaendesha na kutapika damu pasipo kuwa na sumu mwilini,” alisema mtu huyo.

DAKTARI AWAASA MASTAA
Katika hatua nyingine, daktari huyo aliwashauri mastaa wengine kuwa makini kwani mara kadhaa amepata kesi za namna hiyo ambapo wanakunywa pombe vilabuni usiku huku wakiwa katika dozi ya ugonjwa fulani.


Msanii JB akiweka shada la maua wakati wa mazishi ya Adam Kuambiana.

“Mimi nawaambia ndugu zangu, hasa mastaa waache tabia ya kunywa pombe wakiwa katika dozi, starehe zipo tu. Ni vyema wakawa wanauliza kwa wataalam wa afya pindi wanapokuwa wamemeza dawa za aina yoyote, nguvu ya dawa inatofautiana kulingana na ugonjwa husika na muda wa kukaa mwilini,” alisema daktari huyo.

DAKTARI MUHIMBILI ANENA
Ili kuzidi kupata undani wa mazingira ya kifo cha Kuambiana, Amani lilimtafuta daktari mwingine mtaalam wa magonjwa ya binadamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Naye kwa sharti la kutotaja jina alieleza madhara ya mtu kunywa pombe akiwa kwenye dozi.


Mke wa marehemu Janeth Rithe ambaye ni Diwani Kata ya Kunduchi (Chadema), akiweka shada la maua kwenye kaburi la mumewe.

“Unapokunywa dawa hususan hiyo fansidar, inakaa katika mwili kwa takriban siku saba hivyo mgonjwa anapokunywa pombe ndani ya siku hizo, pombe inapochanganyika na dawa katika mzunguko wa damu hugeuka kuwa sumu na mgonjwa ana uwezekano wa kupoteza maisha endapo asipowahishwa hospitalini,” alisema daktari huyo na kuongeza:

“Wengi huwa wanajisahau na kunywa pombe kabla ya siku saba lakini wengine huwa wanakunywa pombe makusudi pale tu wanapoanza kupata ahueni ya ugonjwa pasipo kutambua nguvu ya dawa bado ipo mwilini mwake na madhara yake ndiyo hayo.”


Mabaunsa na wasanii wenzake wakimnyanyua JB, baada ya kuzidiwa na kudondoka chini.

JB AANGUKA GHAFLA, AZUA HOFU
Wakati shughuli za kuaga mwili zikiendelea juzi, Jumanne katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar, nguli wa filamu nchini ambaye alikatisha ziara yake ya kikazi nchini Uturuki kwa ajili ya kuja kumzika Kuambiana, Jacob Steven ‘JB’, alipewa kipaza sauti ili amzungumzie marehemu ambapo akiwa katikati ya kuongea alianguka ghafla.

Marehemu Adam Kuambiana enzi za uhai wake.

Umati wa watu uliokusanyika viwanjani hapo uliingia hofu na kushindwa kuelewa amepatwa na nini lakini haikuchukua muda mrefu akasaidiwa na watu na kuendelea na shughuli nyingine.

MASTAA WAONGOZA KWA VILIO
Mastaa mbalimbali wa Bongo Movies wakiongozwa na Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, Aunt Ezekiel, Blandina Chagula ‘Johari’, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ waliongoza kwa kulia viwanjani hapo hadi walipofika makaburini, Kinondoni.

Msanii wa Filamu Bongo, Jini Kabula akiaga mwili kwa machungu.

Mbali na mastaa hao kuangusha vilio, Mkurugenzi wa Aset, Asha Baraka alijikuta akishindwa kuaga kwa kuhofia kuuona mwili wa marehemu na kudai huwa akitazama maiti anamuota kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Marehemu Kuambiana ambaye alikuwa nguzo muhimu katika ‘ku-dairekti’ filamu, alipatwa na mauti katika Gesti ya Silvarado, Sinza- Kwaremmy jijini Dar. Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.


Davina akibebwa baada ya kuzidiwa wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Adam Kuambiana kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

MASWALI 5 KIFO CHA MENEJA EWURA

JAMBO limezua jambo! Maswali matano ya msingi yameibuka kufuatia kifo cha aliyekuwa Meneja Biashara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Julius Gashaza kilichotokea hotelini katika mazingira ya kutatanisha muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar akitoka Dodoma ambako alihojiwa na Kamati ya Bunge ya Bajeti, Amani limeyanasa.


Meneja Biashara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Julius Gashaza enzi za uhai wake.

Habari za kiintelijensia zilidai kwamba marehemu Gashaza ndiye aliyekuwa na majukumu ya kupanga bei za mafuta kila mwezi, alikuwa mjini Dodoma kwa siku mbili, Ijumaa na Jumamosi iliyopita kuhusu kuweka wazi kiwango cha mafuta kinachoingizwa nchini, mgawo wa fedha unaotolewa na Ewura kwenda kuhudumia umeme katika vijiji (Rea) na fedha za mfuko wa barabara.

Jumapili iliyopita, meneja huyo alikutwa amekufa kwenye Hoteli ya Mwanga Lodge iliyopo Yombo-Vituka, wilayani Temeke jijini Dar na kusadikiwa kuwa alijinyonga kwa tai kwenye nondo za dirisha la chooni katika chumba Na. 113.Mwandishi wetu alifuatilia kwa karibu tukio hilo la kusikitisha na kubaini mambo kadha wa kadha.


Hii ni Hoteli aliyodaiwa kulala Meneja huyo wa Ewura.

NYUMBANI KWA MAREHEMU

Jumatatu iliyopita mwandishi wetu alianza kwa kufika nyumbani kwa marahemu lakini hakuna aliyekuwa tayari kutoa ushirikiano mwa mwanahabari wetu.
Baada ya hapo, mwandishi wetu alikwenda kwenye hoteli hiyo ambako ndiko alikopata maswali hayo matano yenye kuumiza kichwa.

Mhudumu mmoja wa hoteli hiyo ambaye aliomba hifadhi ya jina, alisimulia mazingira yote ya kifo cha meneja huyo, alisema:

“Usiku wa kuamkia siku ya tukio, marehemu alikuja hapa hotelini akiwa ameongozana na watu wanne. Wanawake wawili na wanaume wawili akiwemo yeye marehemu.
“Nilisikia wale wanawake mmoja alikuwa mke wa marehemu, mwingine mke wa rafiki wa marehemu. Wakachukua chumba, wakaingia ndani wote.


Chumba alichodaiwa kulala Meneja wa Ewura.

“Baada ya muda, walitoka watatu. Mke wa marehemu, rafiki yake na mke wa rafiki yake.
“Kwa hiyo inamaanisha ndani ya chumba alibaki marehemu, maana si waliingia wanne na wametoka watatu!

“Tulilala! Asubuhi alikuja yule rafiki wa marehemu akasema anaomba kusaidiwa kumwona marehemu maana amekwenda kugonga lakini hajaamka na mlango umefungwa.

“Tulikwenda wote, kufika kweli mlango ulifungwa. Ikabidi tuchukue funguo nyingine kufungua.
“Hakuwemo chumbani na kwenye kitanda palionesha alama ya mtu kukaa tu si kulala kwani palitengeneza duara alipokaa.

“Kwenda chooni ndipo tukamkuta amekufa kwa kujinyonga kwa tai.”
Alisema kwamba ndipo taratibu za kuwaita polisi zilifuata.


Hiki ni choo alichokutwa meneja huyo.

MANENOMANENO YA WATU
Kufuatia hali hiyo, kumeibuka maneno mengi. Wengine wanadai marehemu alinyongwa na wabaya wake, wapo wanaosema alijinyonga kufuatia uchungu wa kutishiwa maisha na wabaya wake kuhusu kazi.

Wengine wakaenda mbele zaidi kwa kudai kuwa wanyongaji hao walimfuatilia kwa muda mrefu siku ya tukio.

MASWALI MATANO
Swali la kwanza: Kama kweli marehemu alinyongwa ni kwa nini mlango ulikutwa umefungwa kwa ndani? Je, mnyongaji alitokaje baada ya kutekeleza mauaji hayo?


Meneja Gashanza (mwenye kofia) akiwa kazini enzi za uhai wake.

Swali la pili: Kama kweli marehemu alinyongwa, kwa nini kitandani kulikutwa na alama ya mtu kukaa tu na kusiwepo kwa dalili za mapambano au purukushani?

Swali na tatu: Kama kweli alijinyonga mwenyewe ni kwa nini iwe kipindi hiki ambacho inadaiwa alipokea vitisho kutoka kwa wabaya wake kwamba atauawa?
Swali la nne: Uamuzi wa kuchukua chumba kwenye hoteli hiyo ulitoka kwa nani? Marehemu mwenyewe au? Kama alishauriwa, aliyemshauri ana cha kujibu?

Swali la tano: Kama kulikuwa na matatizo ya kikazi kama ilivyodaiwa, basi Mkurugenzi Mstaafu wa Ewura, Haruna Masebu atakuwa anayajua hivyo angeweza kusaidia kuyasema.

Swali lingine ambalo lingeweza kuongeza idadi ni juu ya uwezekano wa kuingizwa kwa funguo nje wakati ya ndani ilizungushwa lakini imebainika kwamba baada ya funguo kufungwa na mlango kuwa ‘lokdi’, funguo hiyo huwa ‘luzi’ tena hivyo mwenye funguo nje anaweza kuisukuma na kuingiza nyingine.

ALIWAHI KUSIAIDIA GLOBAL KUPATA KIBALI CHA KAMPUNI YA KUINGIZA MAFUTA
Marehemu atakumbukwa na uongozi wa Kampuni ya Global Publishers kwani aliwahi kuisaidia kupata kibali cha kuingiza mafuta nchini bila mizengwe wala kutaka shukrani.

Kwa mujibu wa Meneja wa Masoko wa Global Publishers na Kampuni ya Shigongo Oil, Benjamin Mwanambuu, marehemu alikuwa akifanya kazi yake kwa kufuata utaratibu na sheria.

“Kwa kweli nilimfahamu marehumu Gashaza wakati wa kutafuta kibali cha kungizia mafuta katika Kampuni ya Shigongo Oil. Alikuwa mtu mwema sana, asiyetaka njia za uchochoro. Kila hatua ilikuwa ya haki na uwazi,” aliema Mwanambuu.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Engelbert Kiondo alikiri kutokea kwa tukio hilio akisema ameshaingiza ‘vijana’ wake kuchunguza ukweli wa tukio hilo la kujinyonga au kunyongwa.

Mwili wa marehemu Gashaza uliagwa juzi nyumbani kwake, Yombo-Vituka, Dar na kusafirishwa Ngara, Kagera kwa mazishi. Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.

Monday, May 19, 2014

ANGALIA PICHA MWILI WA ADAM KUAMBIANA UKITOLEWA MOCHWARI MUHIMBILI





Mwili wa Marehemu Adam Kuambiana ukiwa ndani ya gari la kubebea maiti baada ya kuchukuliwa moshwari Muhimbili, unapelekwa nyumbani kwake, Bunju, Dar ambako utalala huko kabla ya kuagwa Viwanja vya Leaders na kuzikwa Kinondoni, kesho.


Waombolezaji wakiwa wamelifungua gari la kubebea maiti ili kuweka jeneza lenye mwili wa Adamu Kuambiana leo mchana.



Waombolezaji wakilia kwa uchungu, mmoja akiwa amedondoka baada ya mwili wa Kuambiana kuwekwa kwenye gari la kubebea maiti nje ya moshwari Muhimbili Dar.


Msanii wa Filamu Bongo, Dude akihojiwa na Global TV On Line nje ya moshwari, Muhimbili.



Mmoja wa wasanii wa Bongo Muvi akihojiwa na Global TV on line.



Dude(kulia), Johari, (katikati) na msanii mwingine wakiwa nje ya mochwari, Muhimbili wakisubiri mwili wa marehemu Adam Kuambiana kutolewa na kusafirishwa kwenda Bunju, Dar leo mchana.

MERCY CHARLES KITUNDU KUZINDUA ALBAMU YAKE YA IMBENI SIFA ZA YESU JUMAPILI 25.05.2014


Saturday, May 17, 2014

KAULI ZA WASANII MBALIMBALI WAKIELEZEA KWA UCHUNGU KIFO CHA ADAM KUMBUANA



Baadhi ya wasanii wa filamu akiwemo Yobnesh Yusuphn(Batuli),Bondi Bin Salim aka Bond, Deogratius Shija na Kulwa Kikumba ‘Dude’wameelezea jinsi walivyopokea kwa uchungu taarifa za kifo cha msanii mwenzao Adam Kumbiana aliyefariki dunia asubuhi ya leo. Wakizungumza leo wasanii hao kwa nyakati tofauti tofauti kila mmoja ameonesha kuguswa na taarifa hiyo huku kila mmoja akielezea jinsi alivyopokea taarifa hizo kwa majonzi makubwa.

Dude
“Adam Kuambiana amefariki kweli,chanzo hakijajulikana zaidi lakini kwa taarifa tulizozipata mwanzo inasemekana asubuhi alijisikia vibaya akaona kama mwili unaishiwa nguvu hivi,kwahiyo watu wakachukua gari kumpelea hospitali ndo akafia kwenye gari. Nawapigia sasa hivi simu Mtitu na Stive Nyerere wanaupeleka mwili hospital, wengi wanasema alianza usiku vidonda vya tumbo.”
Batuli

“Msiba unauma sana, ghafla halafu kijana,inauma sana ninachoweza kuongea kwa sasa hivi, ni swala moja kwanza kukubali matokeo la pili ni kumuombea, ameondoka na sisi tunafuata.”
Bondi
“Kweli na mimi nimesikia hivyo, Adam Kuambiana amefariki akiwa location mitaa ya Sinza, kwahiyo
msiba tumeupokea kwa huzuni kubwa ila tumuombee kwa mungu.” Deogratius Shija “Nimesikitishwa na kifo cha Adam Kuambiana,lakini pengo la Adam Kuambia ni kubwa sana, jamaaa alikuwa jembe kwenye filamu, unajua imekuwa ghafla labda ata angeumwa lakini duh ndiyo hivyo hakuna jinsi tumuachie mungu.”

MERCY KITUNDU ALIYEACHWA NA MUME MWISLAMU NA KUFIWA NA WANAWE WAWILI SASA MUNGU AMEMPA KIBALI CHA KUZINDUA ALBAMU YAKE YA IMBENI SIFA ZA YESU SIKU YA JUMAPILI 25.05.2014

Mungu aweza kufuta aibu ya mtu na kumuweka wa thamani machoni pa watu. Mercy Charles ni mwaimbaji wa nyimbo za Injili na ni mwalimu wa kufundisha kuimba katika kanisa la K.K.K.T hapa jijini Dar es Salaam. Mwimbaji huyu amepitia mapito makali sana katika maisha yake. Kabla hajaolewa alikuwa Mkristo na alipota mume wa Kislamu aliamua kubali dini yake na kuwa Mwislamu. Katika ndoa yake alibahatika kupata watoto wawili, wa kiume na kike. Mume wake aliamua kuongeza mke wa pili na akamfukuza huyu mke wake wa kwanza ambaye ni Mercy Kitundu. Mbali na kuachwa aliweza kupata pigo lingine na kufiwa na watoto wake wawili.

Mercy Charles Kitundu

Mungu aliweza kumrudisha katika dini yake ya zamani ya KIKRISTO. Akiwa katika dini yake hii aliweza kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji katika kanisa lake, na mpaka sasa anamtumikia Mungu kwa uimbaji.

Siku ya tarehe 25.05.2014 anazindua albamu yake ya IMBENI SIFA ZA YESU pale Mbagala za Zakheem karibu na DAR LIVE ukifika hapoa uliza kanisa la KKKT liko barabarani kabisa lina paa la kijani. Tamasha litaanza saa 7:00 mchana na kuendelea na hakutakuwa na kiingilio chochote.


Katika mahojiano aliyofanya katika ofisi za RUMAFRICA, Mercy Charles Kitundu ameeleza maisha yake kabla na baada ya wokovu, matatizo katika ndoa, waimbaji kutokuwa na mshikamano, watumishi kutokuwa na ushirikiano katika kuujenga mwili wa Kristo, malengo yake katika uimbaji, vikwaza alivyopata katika kuandaa albamu yake, kiasi alichotumia kumaliza albamu yake, maisha yake katika ndoa ya Kiislamu, katoa moni yake na mambo mengi.


Mawasiliano ya Mercy Charle Kitundu ni
+255 756 248 282 au +255 712 502 020
www.mercykitundu.blogspot.com

SASA WAWEZA KUSIKILIZA KILE MERCY KITUNDU ALICHOKIONGEA KATIKA OFISI ZA RUMAFRICA SINZA AFRIKASANA.

WIMBAJI WATAKAO KUWEPO NI KAMA HAWA WAFUATAOKUWEPO KATIKA TAMASHA ZA UZINDUZI WA ALBAMU YAKE NI KAMA WAFUATAO.

Kutakuwa na waimbaji wengi sana kama BAHATI BUKUKU, MADAM RUTI, ENOCK (ZUNGUKA ZUNGUKA), JULIETH DOUGRAS, SARAH MVUNGI, MAGRETH SEMBUCHE, MC JERRY, MERCY JACOB CHENGULA, FURAHA ISAYA, TUMAINI NJOLE, LEA AMOSI na wengine wengi.

MWILI WA MSANII WA BONGO MOVIE ADAM KUAMBIANA WAHIFADHIWA MHIMBILI


Mwili wa Marehemu Adam Kuambiana ukiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuhifadhiwa leo mchana.

Rais wa Bongo Movies, Steve Nyerere akiwa analia nje ya chumba cha maiti Muhimbuli.


Wasanii wakilia kwa uchungu nje ya chumba cha maiti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mchana wa leo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...