Saturday, November 30, 2013

DIRECTOR WA ENDLESS FAME AJIBU TUHUMU ZA KUKUTWA AKIFANYA UFUSKA NA GARI YA WEMA SEPETU


Baada ya juzi kati kuripotiwa habari ya aliyekuwa producer ama mtengenezaji wa vipindi vya Wema Sepetu Chidi Mohamed kufukuzwa kazi kutokana na kulitumia gari la kampuni kama sehemu yake ya kuvunjia amri ya sita na wadada wa mjini, hatimaye katika pitapita zetu za mtandaoni tuliweza kukutana na kauli ya producer huyo akizungumzia habari hiyo ya yeye kufukuzwa kazi kwenye kampuni ya Endless Fame ya wema sepetu.
Chidi mwenyewe anasema kuwa habari hizo si za kweli na ni kwamba wote walioandika wamepanga kumchafua tuu kwa kuogopa kuwa anaweza kuyaniika mambo mazito yanayoendelea huko endless Fame
Kwa mujibu wa chidi anasema kuwa yeye ameondoka kwenye Kampuni hiyo siyo kwa sababu ya uzinzi ndani ya gari kama ilivyoripotiwa bali ni kutokana na sababu hizi kuu mbili.
1. Ameona hamna jipya na wala hamna maendeleo yoyote ndani ya Kampuni hiyo ndio maana ameamua kuondoka
2. Wafanyakazi wa Endless Fame hawalipwi kabisa ndio maana yeye akaamua kujitoa kwani anafanya kazi bure na pia sio yeye peke yake aliyeondoka bali kuna wafanyakazi zaidi ya watatu walioondoka kwenye kampuni hiyo ila nashangaa ni kwanini wameamua kumchafua yeye?

HATIMAYE MWANA FA, AY NA HERMY B WAMALIZA BIFU LEO LA MIAKA MINGI


‘Friends again’, ni maneno yaliyoandikwa na Amani Joachim (Chief Operations Officers wa B’Hits), kwenye ukurasa wake wa facebook na kupost link yenye picha inayowaonesha AY, Mwana FA, na Hermy B wakiwa kwenye picha moja.

Picha hiyo imepigwa (November 29) inamuonesha Producer wa ‘Habari Ndiyo Hiyo’ Hermy B baada ya kumwagia ndoo ya maji katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Leo mchana Hermy B amepost picha akiwa na FA uwanja wa ndege wa J.K na kuandika ‘Bday continues’.

Thursday, November 28, 2013

ATUHUMIWA KUMUUA BOSS WAKE KWA KOSA LA KUULIZWA UMECHELEWA WAPI!






Kijana Daniel Kossam (21) anatuhumiwa wa kumuua bosi wake Bi,Pelesi Chaula (32)ambaye alikuwa akiishinaye nyumba moja huko mtaa wa Ilembo kata ya Iyela mkoani mbeya akiwa chini ya polizi kwenda kuonyesha pesa na simu alivyotumbukiza chooni

Kijana Daniel Kossam (21) anatuhumiwa wa kumuua bosi wake Bi,Pelesi Chaula (32)ambaye alikuwa akiishi naye nyumba moja huko mtaa wa Ilembo kata ya Iyela mkoani mbeya

Daniel alikuwa akiuza duka la vifaa vya pikipiki la bi, Pelesi lijulikanalo kwa jina la 'Twiyanze' lililopo kijiji cha Mbalizi nje kidogo ya jiji la Mbeya.

Chanzo cha ugomvi inadaiwa kuwa ni kuchelewa kurudi nyumbani kijana huyo ndipo Pelesi alipochukua jukumu la kumuuliza jambo lililozua ugonvi katiyao na kusababisha kifo cha bi.Pelesi Chaula.

Kifo cha marehemu Pelesi kimetokana na kupigwa na kitu chenye ncha kali mwilini mwake.

Wakati mauaji hayo yanafanyika mume wa bi Pelesi Chaula alikuwa safarini wilayani Makete mkoani Iringa.

Baada ya mauaji hayo Kijana Daniel alichukua simu mbili za marehemu na simu yake pamoja na fedha kiasi cha 114000/= na kuzitumbukiza chooni kisha alienda kwa jirani kuwajulisha kuwa walikuwa wamevamiwa na majambazi na kwamba wamemuua bosi wake huyo.

Majirani walipofika eneo la tukio walishangaa kuona kuwa hakuana sehemu ya nyumba iliyokuwa imevunjwa, walipo muuliza Daniel alijibu kuwa alisahau kufunga milango, baaada ya majibu hayo waliingiwa na mashaka na kuamua kutoa taarifa polisi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mjumbe wa serikali ya mtaa Bi,Neema Mwasampeta alisema,' Dan alichelewa kurudi na alifokewa sana,nadhani hicho ndiyo chanzo cha ugomvi wao'. aliongeza kuwa alimjua kijana huyo kwa muda wa mwaka mmoja.




Marehemu Bi,Pelesi Chaula (32) enzi za uhai wake



Harakati za kutafuata fedha na simu tatu zilizotupwa chooni na anaetuhumiwa kwa mauaji

Afisa upelelezi wa wilaya Mbeya mtatiro akishukuru wakazi wa mtaa wa iyela kwa ushirikiano utulivu waliouonyesha wakati wa zoezi la kutafuta vidhibiti.

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA VIJANA WA UMOJA WA VIJANA CCM (UVCCM)

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Beji ya Mapambano dhidi ya Ukimwi na Katibu wa Hamasa na Chipukizi Taifa, Paul Makonda, wakati alipokutana na Vijana hao wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wenye lengo la kusambaza ujumbe kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Desemba 1.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Vijana wa UVCCM, baada yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Vijana wa UVCCM, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.

makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Vijana wa CCM, baada ya mazungumzo yao alipokutana nao jana kwa ajili ya kumkabidhi ujumbe kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Desemba 1.

AIRTEL YAWANOA WATANGAZAJI WA RADIO MBALIMBALI LEO


Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akisistiza jambo kwa watangazaji wa vipindi vya redio mbalimbali (hawapo pichani) kuhusu vigezo na masharti vinavyotakiwa kufuatwa kwenye promosheni mpya ya Airtel ya "Mimi ni bingwa" itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kushinda tiketi 2 kila wiki za kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za timu ya Manchester United na mamilioni ya pesa kila siku.Kulia kwake ni ofisa wa matangazo wa Airtel Bw. Abdallah Gunda.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akiwaelezea waandishi wa habari jinsi ya kujiunga na promosheni mpya ya Airtel ya "Mimi ni Bingwa" itakayowawezesha wateja wa Airtel kushinda tiketi 2 za kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za Manchester United kila wiki au mamilioni ya pesa kila siku. Kutoka kulia ni Meneja masoko wa Airtel Upendo Mkini akifuatiwa na meneja msimamimizi wa promosheni hiyo Fatma Ngororo.
Toka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airte Tanzania Bw Jackson Mmbando akibadilishana mawazo na watangazaji wa kipindi cha jahazi bw Musa Huseni (kati) na Ephraem Kibonde mara baada ya mkutano maalum na watayarishaji na waandaaji wa vipindi mbalimbali vya redio kwa lengo la kuwaeleza vigezo na masharti vinavyotakiwa kufuatwa kwenye promosheni mpya ya Airtel Mimi ni bingwa" inayowawezesha wateja wa Airtel kushinda tiketi 2 kila wiki za kwenda kushuhudia mechi mbalimbali za timu ya Manchester United na mamilioni ya pesa kila siku.

WAZIRI MKUU PINDA AMFARIJI MZEE MANGULA KUFUATIA KIFO CHA MWANAYE PETER PHILIP MANGULA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimfariji Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula wakati alipokwenda nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam kumpa pole kufuatia kifo cha mwanaYe, Peter Philip Mangula kilichotokea Novemba 26, kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Wednesday, November 27, 2013

MAITI HUFUKULIWA MAKABURINI ILI KUBADILISHWA NGUO HUKO INDONESIA


Pichani ni baadhi ya wafu waliofukuliwa kaburini na kuvishwa nguo Indonesia.

KILA mwaka huko Tana Toraja, Indonesia, wafu (au maiti) hufukuliwa kutoka makaburini ili kubadilishwa nguo. Watu wa eneo hilo wa kabila la Toraja wana mila za ajabu kuhusu vifo na maisha yanayofuata baada ya mtu kufa.
Wao mtu akifa hutakiwa kuzikwa katika eneo alilozaliwa na si lazima azikwe katika eneo alilofia.
Idadi kubwa ya watu wa eneo hilo ni Wakristo, wanaofuata ni Waislam na wengine ni Wapagani ambao wanajulikana kwa imani au madhehebu ya Aluk To Dolo yaani “Njia ya Mababu”.
Torajan huishi katika maeneo ya milimani na hawataki kujulikana sana katika jamii, japokuwa wana mila na desturi zao zilizoenea katika jimbo la Sulawesi.

MTOTO ARUDISHA PENZI LA MONALISA NA TYSON



NDOA ya mastaa wa filamu Bongo, George Tyson na Yvonney Chery ‘Monalisa’ iliyovunjika kitambo, ilirejewa na uhai wa saa kadhaa katika shughuli ya kumpongeza binti yao mpendwa Sonia baada ya kupata kipaimara.

Mwandishi wetu aliwashuhudia wawili hao wakionekana dhahiri kuweka tofauti zao pembeni na kujali shughuli ya binti yao iliyofanyika Jumapili iliyopita nyumbani kwa mama mzazi wa Monalisa, Suzan Lewis ‘Natasha’, Yombo –Buza, Dar.

Muda wote walionekana wenye furaha na waliketi kwenye meza moja huku Monalisa akionesha heshima wakati wa kumlisha keki Tyson kwa kupiga magoti.

“Hawa jamani wanapendezana sana wakiwa pamoja. Jamani... mtoto wao amerudisha penzi lao. Ingefaa wakafikiria upya na kuona kuna umuhimu wa kurudiana na kumlea pamoja mtoto wao,” mmoja wa wageni waalikwa alisikika akisema.

Katika kuonesha kuwa kweli hawana bifu, Mona aliamua kumtunza mzazi mwenzake noti nyingi za elfu kumikumi zilizokadiriwa kuwa zaidi ya 200,000 ambapo alisema: “Huwa nawashangaa watu wengi wakiwatuza akina mama kwa kuwalea vyema watoto lakini wanawasahau akina baba. Sasa mimi namzawadia baba Sonia kwa sababu bila yeye, mtoto wetu asingekuwepo.”

Tukio hilo lilivuta hisia za watu na kusababisha shangwe kubwa kuibuka katika sherehe hiyo.

Tuesday, November 26, 2013

YALIYOJIRI:MKUTANO WA CHADEMA NA WAANDISHI WA HABARI


Mheshimuwa John Mnyika, Tundu Lissu na Benson Kigailla ndio wazungumzaji wakuu.

Mnyika - amewaleeza waandishi kuwa sekritarieti ya chama ilikaa kikao chake jana kujadili mambo kadhaa ndani ya chama.

Ameeleza kuwa wahusika wamesha andikiwa barua zenye tuhuma zao 11 wanazotakiwa kuzijibu ndanj ya siku 14.

Ameeleza kuwa press conference waliyofanya wamejitungia tuhuma ambazo kimsingi sizo zilizo wavua nafasi zao.

Benson Kigailla anaeleza mikakati inayoendelea kwenye kanda ambayo kimsingi ripoti zililetwa kwenye kamati kuu.

Anasema mpango na programu ya chadema ni msingi pamoja na M4C kanda unaendelea kwa mafanikio makubwa kwani misingi inaendelea kuundwa na mpaka sasa zaidi ya wakunzi elfu tisa kutoka katika kanda mbalimbali wameshafundishwa.

Wakufunzi waliokwisha fundishwa.

Taifa 30

Kanda 40

Majimbo 956

Kata 19,408

Vijiji/Mitaa 72,000

Anaeleza kuwa kuna timu nne zimeundwa kwenda kwenye kanda mbalimbali kukagua misingi iliyokwisha simikwa.

Ziwa Mashariki misingi 3069 kati 7098

Ziwa Magharibi 3840 kati 9757

Kaskazini 3278 kati ya 8417

Juu kusini 2113 kati ya 10,857

Magharibi Kata 235 kati ya kata 315

kanda ya Kati Kata 363 kati ya 495

Kanda Kusini 219 kati ya 387

Kanda ya Pwani misingi 846

Tundu Lissu.

walichokifanya kina Zitto na Kitilla ni "Diversion" mashtaka yao yanatokana na waraka wa kihaini wa mabadiliko ambao ni kinyume na katiba na maadili ya uongozi, kuvuliwa kwao nafasi zao hakuhusiani na mambo ya PAC wala kuuza nafasi zetu za wagombea kwa maccm, wala kutokushiriki kwenye ziara za chama.

anawaambia waandishi, "wamevuliwa nafasi zao na kamati kuu kwa sababu ya waraka wenye nia ovu"

Anasema chadema haijaanza kufanya maamuzi magumu leo, ilishafanya hivyo kwa Dr Walid Kaburu na kwa Chacha Wangwe na mara zote vyombo vya habari vimekuwa vinaandika kuwa CHADEMA yapasuka, mara CHADEMA inakufa lakini kipindi chote haijawahi kufa wala kupasuka, na hata kwenye hili haitakufa kama ikitokea kamati ikiwafukuza.

Lissu alieleza kuwa - Kitilla amepotosha kuwa kamati kuu haina mamlaka ya kumvua yeye nafasi yake ya ujumbe wa kamati kuu maana amechaguliwa na baraza kuu. Amesema Zitto alipaswa kumkumbusha rafiki yake maana yeye (Zitto) alikuwepo kwenye kamati kuu iliyo mvua ukatibu mkuu Dr Walid kaburu, na makamu mwenyekiti bara Chacha Wangwe. kama iliweza kwa Kaburu na Chacha Wangwe (Katibu mkuu na Makamu mwenyekiti) imeweza na kwake pia ambaye hana vyeo hivyo, hivyo aache kupotosha umma kwa makusudi.

Mwandishi mmoja aliuliza kuhusu vurugu za kuchana bendera huko Kigoma, majibu yalikuwa - kurugenzi ya ulinzi na usalama ya chama imewasiliana na viongozi wa chama Kigoma na watalitolea wao taarifa lakini taarifa za awali ni kwamba ulikuwa mpango wa kuigiza ulioandaliwa na watu waliotumwa na wameshajulikana na hatua zaidi ziko chini ya uongozi wa tawi husika.

Monday, November 25, 2013

Mwili wa mwanamamke wakutwa kichakani ukiwa umekatwa kichwa na kufungwa kamba.



Kwenye kijiji cha Nyamira wanakijiji wameamka na kukuta mwili wa mwanamke ukiwa umekatwa kichwa na kutelekezwa pamoja na kufungwa mikono kwa kamba.

Mwili huo ambao unaonyesha kuwa ni mwanamke mwenye miaka kati ya 25 hadi 35 amekutwa umevaa jeans pamoja blouse nyeusi na kutupwa pembeni ya kijito cha maji mida ya saa 12 na nusu asubuhi.

Wanakijiji walishtuka na tukio hilo na kusema kwamba ni kitu cha ajabu kwenye kijiji chao na polisi wa Kenya wametangaza familia yoyote itakayoona kuna mtu amepotea nyumbani kwao atoe taarifa.

KILIMANJARO STARS WAAGWA HOTELI YA TANSOMA


Katibu wa Baraza la Michezo Tanzania Henry Lihaya(kushoto) akiwakabidhi Bendera ya Taifa kocha wa Kilimanjaro Stars Kim Poulsen na kapteni Kelvin Yondani. 
 
Kilimanjaro Stars leo wameagwa rasmi katika Hoteli ya Tansoma, Jijini Dar tayari kuelekea nchini Kenya kushiriki mashindano ya Chalenji yanayotarajiwa kuanza siku ya Jumatano ya wiki hii. Kilimanjaro Stars wanaondoka leo kuelekea nchini humo.
Mjumbe wa TFF Godfrey Nyange 'Kaburu'(kushoto) wa katikati ni kocha wa Kilimanjaro Stars Kim Poulsen na Katibu wa Baraza la Michezo Tanzania Henry Lihaya(kulia).
Nahodha wa timu ya Kilimanjaro Stars Kelvin Yondani (kulia) akiongea na waandishi wa habari leo.
Wachezaji wa timu ya Kilimanjaro Stars.

JANUARY MAKAMBA APEWA MAKAVU LIVE NA LADY JAY DEE


Lady Jaydee aka Anaconda amemshukia January Makamba live mara baada ya mheshimwa huyo kuandika post inayo husu kupromte wamamuziki na wasanii wa Tanzania kupitia twitter yake. shuka nayo:




Sunday, November 24, 2013

HAYA NDIYO YALIYOJILI SHOO YA P-SQUARE DAR












Ooooo, mambo ya Diaomond haya sasa!!!


...ilikuwa ni shoo Live ya ukweli!
Peter na Paul Okoye 'wakilivamia' kiukweli jukwaa la Leaders

JAYDEE,PROFESA JAY,BEN POL & JOH MAKINI KWENYE STEJI


Mashabiki wakipagawa na shoo ya P-Square.

......baada ya shoo kali ya masaa matatu, sasa inatosha Dar es salaam..asante sana...’tank yo! tank yo’!!!
Joh Makini akilitawala jukwaa.
Nikki wa Pili (kushoto) na G Nako wakifanya yao stejini.
Kundi la Weusi likiongozwa na Joh Makini likishambulia jukwaa la Leaders Club kabla P-Square hawajapanda usiku huu.
PMwanamuziki Joseph Haule 'Profesa Jay' akiwapagawisha vilivyo mashabiki waliohudhuria shoo ya P-Square Live in Dar ndani ya Viwanja vya Leaders Club vilivyopo Kinondoni jijini Dar.
Nyomi HAPO JUU baada ya kuikubali vilivyo shoo ya Profesa Jay.
LMwanamuziki Judith Wambura 'Lady Jaydee' au 'Anaconda' akiwapagawisha mashabiki wake waliohudhuria katika Viwanja vya Leaders Club usiku huu katika shoo wa wakali P-Square.
Watu... Jideeeeeeeeeeee...
Machozi Band nao walikuwepo kumback up Jide.
Mwanamuziki Ben Pol akiwasha moto katika steji ndani ya Viwanja vya Leaders katika shoo ya P-Square Live in Dar.
Nyomi ikifuatilia shoo ya Ben Pol.
Ben Pol akiimba sambamba na mwanadada.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...