Thursday, October 31, 2013

BAADA YA KUPOTEA SIKU 3 MTOTO AKUTWA AKIWA AMEFARIKI NDANI YA SHIMO LA CHOO CHA JIRANI


Mwili wa Mtoto Joshua Isack (4) ukichukuliwa na polisi.



Hili ndilo shimo alimokutwa marehemu Joshua.

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Mtoto Joshua Isack (4) aliyepotea nyumbani kwao akiwa anacheza na watoto wenzie kwa siku tatu akutwa akiwa amefariki dunia ndani ya shimo la choo cha jirani na kuzua maswali ya sintofahamu kwa wazazi na majirani.

Tukio hilo la kuonekana kwa mtoto huyo lilitokea jana majira ya saa Kumi jioni katika Mtaa wa Nyibuko Pambogo kata ya Iyela Jijini Mbeya baada ya juhudi za wazazi na majirani kushirikiana kumtafuta na kumpata akiwa amepoteza maisha ndabi ya shimo la choo.

Akizungumza kwa uchungu na masikitiko makubwa baba mzazi wa marehemu Isack Daniel ambaye ni mfanyakazi wa Mamlaka ya Maji Mbeya alisema Mtoto wake huyo wa kiume akiwa anacheza na wenzie jumatatu ya Oktoba 28, Mwaka majira ya saa 12 jion lakini alitoweka katika mazingira ya kutatanisha.

Alisema baada ya kuona giza linaingia na mtoto hajarudi alianza kumtafuta katika kila eneo akishirikiana na baadhi ya ndugu na majirani lakini hakufanikiwa kumwona kwa siku hiyo ambayo kesho yake akiwa ni viongozi wa mtaa walienda kutoa taarifa kituo cha Polisi cha Kati Mbeya Mjini.

Mzazi huyo aliendelea kusema baada ya kutoa taarifa polisi bado waliendelea na juhudi za kumtafuta huku Ubalozi ukiunda kikosi maalumu cha kufanya msako wa nyumba hadi nyumba ambapo baada ya kupita katika nyumba ya jirani alipokutwa marehemu katika shimo la maji machafu walipatwa na wasi wasi baada ya kuona kuna mabadiliko ya mbao zilizokuwa zimefunika shimo hilo.

Alisema awali walivyopita siku moja kabla waliona shimo hilo likiwa limefunikwa kwa mabanzi yaliyochakaa lakini siku ya pili yake asubuhi walikuta kukiwa na mabanzi mapya kuashiria kuna ukarabati umefanyika hali iliyowapa wasi wasi na kulazimika kulifunua shimo hilo na kumkuta marehemu akiwa amepoteza maisha ndani ya shimo hilo.

Alisema aliyegundua kuwepo kwa mtoto ndani ya shimo ni ndugu yakle alikuwa katika msako wa nyumba kwa nyumba na ndipo alipompigia simu akiwa kazini nay eye kutoa taariofa polisi na kwenye Serikali ya Mtaa ambapo walianza kufanya juhudi za kumtoa lakini walikwama hali iliyowalazimu kuomba msaada kwa kikosi cha Zimamoto na Uokoaji waliofanikiwa kumtoa majira ya saa Kumi jioni.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Nyibuko Pambogo kata ya Iyela Mage Makwenda alisema akiwa ofisini kwake alipokea taarifa za kupotea kwa mtoto katika mazingira ya kutatanisha lakini wakiwa katika juhudi za kumtafuta ndipo walioteuliwa kufanya upelelezi na msako mkali walipotoa taarifan za kuonekana kwa mtoto akiwa am,efariki dunia ndani ya shimo la maji machafu.

Alimtaja mmiliki wa nyumba hiyo kuwa ni Gesho Kibonde (43) mkazi wa Mtaa wa Nyibuko kata ya Iyela Jijini hapa ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano pamoja na mkewe.

Kwa upande wake majirani na wakazi wa mtaa huo ambao hawakutaka majina yao kuandikwa walisema tukio hilo lina utata mkubwa kwa sababu baada ya mtoto kuonekana ndani ya shimo baadhi yao walifanikiwa kuchungulia na kumkuta marehemu akiwa amesimamishwa mithiri ya kutumbukiwa na mtu.

Mashuhuda hao waliendelea kusema kama mtotio angekuwa ametumbukia kwa bahati mbaya akiwa anacheza na wenzie angeonekana kuumia baadhi ya viungo lakini haikuwa hivyo pamoja na kuonekana kufa maji machafu ndani ya shimo hilo basi tumbo lake lingejaa lakini hali aliyokutwa nayo marehemu ni tofauti.

Hata hivyo wengine wamelihusisha tukio hilo na imani za kishirikina kwa madai kuwa aliyewaonesha kuwepo kwa mtoto ndani ya shimo hilo ni babu kutoka Mwakaleli( mganga)ambaye alifuatwa na baadhi ya watu ili kusudi awaoneshe mtoto na ndipobabu huyo alipowaambioa warudi katika nyumba ya jirani watamkuta akiwa hai.

Walisema baada ya kurudi na kutafuta katika eneo hilo waliokuta akiwa amekufa kitu ambacho waliamini ni kuchelewa kufika na kuligundua eneo lakini wanrwahi huenda wangemkuta marehemu akiwa mzima kabisa. Aidha wakati zoezi la kumtoa marehemu ndani ya shimo hilo kwa ushirikiano wa Jeshi la Polisi, Zimamoto na Uokoaji pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Mbeya( Mbeya uwsa) vilio vilitawala eneo hilo kutoka kwa wanawake walioshindwa kujizuia huku wengine wakipoteza fahamu na kulazimika kupewa msaada wa kupepewa.

BINTI WA MIAKA 17 APOTEZA MAISHA KISA NI FACEBOOK


Binti wa miaka 17 nchini India katika jiji la Parbhani amejiua baada ya wazazi wake kumkataza asitumia ukurasa wa Facebook ili apate muda wa kuzingatia masomo aliyokuwa akishindwa vibaya darasani tofauti na ilivyokuwa kabla yajaanza kutumia Facebook ambapo alikuwa akifaulu.

Aishwarya Dahiwal alikutwa ananing'inia chumbani kwake baada ya kuzuka mabishano baina yake na wazazi wake ambao
walikuwa wanakerwa na muda mwingi anaoutumia kwenye mtandao wa Facebook na mazungumzo marefu kwenye simu yake ya mkononi.

Gazeti tando la habari za teknolojia, Gawker limeripoti kuwa marehemu aliacha ujumbe usemao kuwa asingweza kuishi bila mitandao ya kijamii na moja ya yaliyoandikwa humo ni pamoja na kuuliza, "Je, Facebook ni mbaya hivyo?" "Siwezi kuishi katika nyumba yenye vizuizi vya aina hii na siwezi kuishi bila Faceboook" na hivyo kuwalaumu wazazi wake kwa hatua ya kujiua aliyoichukua.

Kama ilivyo kwa wazazi wowote ambao kwa kawaida wameyaona maisha na kufahamu mbinu za kukabiliana nayo, walikuwa na nia njema ya kutaka kumsaidia mtoto wao aweze kufanikiwa lakini mabadiliko ya kila kizazi yanayokuja na changamoto zake ambazo hazina vigezo wala vielelezo vya namna ya kumsaidia mtoto akabiliane navyo vyema hali akiyamudu maisha kwa uwiano, walijikuta katika huzuni ya kulazimika kukubaliana na jambo ambalo hawakutarajia lingetokea.

Bila shaka ujio wa internet umebadili maisha ya vijana na familia kwa ujumla. Pamoja na kuwa na faida nyingi kwa wale wanaojua namna ya kuitumia vyema, bado madhara na hasara zake ni kubwa ambazo zinaonekana dhahiri kwenye mahusiano ya aina zote iwe kikazi, kifamilia, kijamii au hata kutoka kwa mtu msiyefahamiana kabisa ila kwa kuwa amekuona kwenye moja ya mitandao ya kijamii, anaweza kukutisha na hata kukudhuru.

Jirani yangu alinisimulia jinsi rafiki yake alivyoibiwa nyumbani kwake baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa baada ya uchovu wa kazi wiki nzima, amekwenda kubarizi ufukweni na atarudi majira ya jioni hivi, kwa kuwa anwani yake ilikuwa kwenye wasifu wake (profile details) basi taarifa hizo zikawa maelezo ya kutosha kwa wezi kufanya watakavyo.

HIVI NDIVYO MWILI WA MAREHEMU BABA AKE WEMA ULIVYOZIKWA ZANZIBAR



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Padri wa Kanisa Katoliki la Minara miwili Mjini Zanzibar Cosmas Amani Shayo, alipowasili katika eneo la Mazishi ya Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja jana.
Jeneza la Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,likiwa limebebwa na Askari Polisi na kulifikisha katika kaburi lake yalipofanyika mazishi kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja jana.
Padri wa Kanisa Katoliki la Minara miwili Mjini Zanzibar Cosmas Amani Shayo, akiuombea mwili wa marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja jana.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,ukitemshwa katika kaburi wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja jana.
( PICHA RAMADHAN OTHMAN IKULU )

Wednesday, October 30, 2013

RAIS WA ZANZIBAR AHUDHURIA SHUGHULI ZA MAZIKO YA BABA AKE WEMA SEPETU


 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akiuwaga Mwili wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani,Mnazi mmoja Mjini Unguja leo asubuhi,Marehemu alifariki juzi Jijini Dae es Salaam,na atazikwa Kijiji kwao Mbuzini Wilaya Magharibi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimpa pole Mjane wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu,Mama Miriam Sepetu,alipofika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani,Mnazi mmoja Mjini Unguja,kuuaga mwili wa Marehemu leo Asubuhi.{Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.}

Baadhi ya Wananchi mbali mbali wakiwa katika sehemu maalum nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani,Mnazi mmoja Mjini Unguja,wakisubiri kuuaga mwili wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu,leo asubuhi ambapo utazikwa Kijiji kwao Mbuzini Wilaya Magharibi.{Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.}

BABU SEYA,PAPI KOCHA KUACHIWA HURU KESHO?



Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson Nguza 'Papii' wakiwa na nyuso za furaha wakati wakitoka katika Mahakama ya Rufaa baada ya majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kusikiliza maombi yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia hukumu iliyoitoa mwaka 2010.

Nyuso za matumaini.......

Johnson Nguza 'Papii' akibusu mkono wake baada ya kuibusu ardhi mara baada ya kutoka mahakamani.

Papii akinyoosha mkono juu kama ishara ya kumshukuru mungu.

Waandishi wa habari wakiwa chini wakati wa harakani za kuchukua matukio mahakamani hapo.


Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson Nguza wakati wakitoka mahakamani.

Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.

Watu waliohudhuria mahakama hapo wakifuatilia kesi hiyo.

Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.

Mahakamani.
Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson Nguza wakiteta jambo na wakili wao, Mabere Marando.

MWILI WA BABA MZAZI WA WEMA SEPETU UNATARAJIWA KUZIKWA MCHANA HUU ZANZIBAR



Picha ya Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu enzi za uhai wake

Mh. Jaji Warioba akisaini kitabu cha Maombolezo leo mchana nyumbani kwa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akisaini kitabu cha maombolezo leo October 29, 2013 nyumbani kwa marehemu Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu

Mama Gertrude Mongella akisaini kitabu cha maombolezo kwenye msiba wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu nyumbani kwake Sinza Mori leo October 29, 2013

Mh. Jaji Warioba na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernard Membe wakibadilishana mawazo kwenye msiba wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo October 29,2013



Baadhi ya viongozi waliofika msibani kwa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu.

Mtoto mkubwa wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu, Aman Isaac Sepetu akizungumza jambo na mwandishi wa habari, Mkwaia wa Kuhenga leo October 29, 2013 nyumbani kwa Marehemu

Mtoto wa marehemu akimsalimia mama baada ya kufika msibani hapo leo mchana

Mama akiwa na mwanae baada ya kufika msibani

Wema Sepetu (katikati) akiongea na Dada yake (wa kwanza Kushoto) na (kulia) ni mama yao.

Mmoja wa watoto wa marehemu Nuru Sepetu alishindwa kujizuia na kuanza kulia na kupelekea watu wengine kuanza kulia kwa majonzi
Mwili wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu ukifikishwa nyumbani kwake

RAISI WA CAF AMPONGEZA JAMAL MALINZI

Jamal Malinzi, Rais mpya wa TFF.


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou amempongeza Jamal Malinzi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.

Katika salamu zake kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya CAF na familia ya mpira wa miguu Afrika, Rais Hayatou amesema uchaguzi huo unampa Rais Malinzi fursa ya kuupeleka mbele mpira wa miguu nchini Tanzania.

Amesema CAF ina imani uwezo wake katika uongozi, uzoefu na ujuzi katika mpira wa miguu havitausaidia mpira wa miguu Tanzania pekee bali Afrika kwa ujumla, na kuongeza kuwa ataendeleza ushirikiano uliopo ili kuwanufaisha zaidi vijana wa bara hili.

Rais Hayatou amemtakia Rais Malinzi kila la kheri katika kipindi chake cha uongozi na kumhakikishia kuwa CAF iko pamoja naye katika kusukuma mbele gurudumu la kuendeleza mpira wa miguu.

WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI NSSF WATEMBELEA MIRADI YAO‏



Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na maofisa wa NSSF wakitembelea mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na maofisa wa NSSF wakitembelea mradi wa nyumba za bei nafuu eneo la Mtoni Kijichi.

Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi Karim Mattaka (wa kwanza kulia waliokaa mezani) akitoa taarifa fupi kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii na maofisa waandamizi wa taasisi hiyo juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni.
Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi Karim Mattaka (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii na maofisa waandamizi wa taasisi hiyo juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na maofisa wa NSSF wakiteremka kwenye gari katika moja ya miradi ya taasisi hiyo walipotembelea jana.

Mmoja wa maofisa wa juu na mhandisi kutoka NSSF akifafanua jambo kwa wajumbe wa bodi.

Mfisa Mradi msimamizi na Msanifu wa NSSF, Deogratias Mponeja (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo juu ya mradi wa awamu ya tatu ya ujenzi wa nyumba nafuu kwa wajumbe.


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (wa pili kulia) akiwa na Eunice Chiume wakizungumza jambo katika ziara ya wajumbea wa Bodi ya NSSF kutembelea miradi jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi wa Mradi na Msanifu Majengo wa NSSF, Mkurugenzi wa Mipango, Miradi na Uwekezaji wa NSSF, Yacoub (aliyesimama) akitoa taarifa fupi juu ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa wajumbw wa bodi.

Na Joachim Mushi, Dar es Salaam

WAJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wamefanya ziara ya kutembelea baadhi ya miradi kadhaa inayotekelezwa na shirika hilo iliyopo jijini Dar es Salaam. Miradi iliyotembelewa katika ziara hiyo ni pamoja na ule wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu uliopo eneo la Mtoni Kijichi na ujenzi wa Daraja la Kisasa eneo la Kigamboni.

Akitoa taarifa fupi kwa wajumbe wa bodi ya NSSF wakiwa eneo la ujenzi wa nyumba za bei nafuu na za kisasa eneo la Mtoni Kijichi, Mkurugenzi wa Mipango, Miradi na Uwekezaji wa NSSF, Yacoub Kidula alisema eneo hilo linatekelezwa kwa awamu mbili za ujenzi wa nyumba aina mbalimbali.

Alisema awamu ya pili ambayo iliendelea baada ya kukamilika ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 85, imetekelezwa kwa ujenzi wa nyumba 215 eneo la Mtoni Kijichi mradi ambao tayari umekamilika na nyumba zimeanza kuuzwa kwa wanachama wa NSSF. Alisema nyumba 200 tayari zimekamilika huku 15 zilizosalia zikiwa katika hatua za mwisho kukamilika.

Alisema tayari Shirika hilo limeanza kutekeleza ujenzi mwingine wa awamu ya tatu utakaowezesha ujenzi wa nyumba za kisasa na bora zaidi zenye uwezo wa kuchukua familia 820 zikiwa na ghorofa moja huku zikiwa zimeboreshwa zaidi kihuduma ukilinganisha na zilizojengwa awali.

Aidha akifafanua juu ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu zinazoendelea kujengwa na NSSF, alisema mbali na kuwa za bei ya chini zinahuduma muhimu za kijamii kama umeme, maji, mfumo mzuri wa kuifadhi maji taka, eneo la nje la ziada pamoja na vifaa vingine zikiwemo feni vyumba vyote, mfumo wa maji ya moto kwenye mabafu na sakafu ya kisasa 'tiles'.

Alisema nyumba zinazojengwa zinaukubwa na idadi ya vyumba tofauti kulingana na maitaji ya mteja, yaani kuanzia vyumba viwili hadi vitatu vya kulala huku vyote vikiwa na sebule, jiko, choo pamoja na stoo. Aliongeza kuwa milango na madirisha yamejengwa kwa vioo na chuma (nondo) ili kuimarisha zaidi kiusalama huku jiko likiwa na kabati maalumu na za kisasa kwa ajili ya kuifadhia vitu.

Kidula alisema nyumba ya chini itauzwa takribani sh milioni 66 za kitanzania bei hiyo ikiwa ni pamoja na VAT. Wajumbe wa bodi pia walitembelea mradi mkubwa wa NSSF wa ujenzi wa daraja la Kigamboni ambao unafanywa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Serikali.

Akitoa taarifa za maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, Meneja Mradi huo, Mhandisi Karim Mattaka alisema licha ya ujenzi huo kuendelea vizuri kwa sasa zipo changamoto kadhaa za ujenzi ambazo zilijitokeza hivyo kushughulikiwa mara moja.

Alisema daraja hilo la kisasa litakalokuwa na njia (barabara sita) yaani tatu za kwenda Kigamboni na tatu za kurudi linatarajiwa kuunganishwa kisasa na barabara ya Mandela huku likiwa na njia za kutosha kuzuia msongamano wa magari. Akizungumzia ziara hiyo ya Wajumbe wa Bodi, Meneja Uhusiano Kiongozi, Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume alisema ni ziara ya kawaida ya wajumbe hao kukagua miradi ya taasisi hiyo na huenda ziara hiyo ikawa na manufaa ya punguzo la riba kwa wanachama wanunuzi wa nyumba hizo.

TIMU YA SIMBA SC.VS KAGERA SUGER KUKIPIGA KESHA




Baadhi ya wachezaji wa Simba SC.

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi ya 12 kesho (Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Viingilio katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.

Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...