Wednesday, July 31, 2013

HALIMA MDEE AFUNGUKA KUHUSU WAUZA UNGA---MADAWA YA KULEVYA




MFANYAKAZI WA KAMPUNI YA MWANANCHI APIGWA RISASI....YAINGIA NA KUTOKEA UPANDE WA PILI



Jessica Ngassa akimuhudumia mumewe, Jackson Ngassa ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Idara ya Usambazaji wa Magazeti aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi na majambazi Jumamosi usiku jijini Dar es Salaam.

Watu ambao wanasadikiwa kuwa ni majambazi wamemjeruhi kwa risasi mfanyakazi wa Idara ya Usambazaji ya Mwananchi Communications Limited, Jackson Ngassa.
Tukio hilo lilitokea juzi Jumamosi saa 4 usiku eneo la Tabata Matumbi baada ya watu hao kumfuatilia Ngassa tangu alipokuwa anatoka ofisi za Mwananchi eneo la Tabata Relini.

Akizungumza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (Moi), Ngassa alisema wakati akitoka ofisini siku hiyo aliona pikipiki tatu zikiwa nyuma yake lakini hakuhisi kama zilikuwa zinamfuata mpaka walipofika taa za kuongozea magari za Tabata Dampo.

“Nilipofika Tabata Dampo nilihisi kufuatiliwa kwa sababu kila nilipopunguza mwendo nao walipunguza mpaka nilipofika Matumbi ndipo nikasikia wakiniambia simama haraka na kisha wakapiga risasi moja ambayo ilitoboa tanki la mafuta la pikikipiki,” alisema Ngassa.

Alisema baada ya kuona hivyo akataka kukimbilia Benki ya Access iliyoko eneo hilo la Matumbi lakini kabla hajafanya hivyo pikipiki nyingine ilimzuia kwa mbele na ghafla akasikia risasi ambayo ilipasua sehemu ya goti mguu wake wa kulia.

Hata hivyo, Ngassa alisema begi hilo halikuwa na pesa zozote zaidi ya kadi ya benki na magari ya kuchezea watoto aliyowanunulia watoto wake.

Kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa kuunganisha mifupa iliyovunjika kwani risasi aliyopigwa iliingia na kutoka upande wa pili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari alikwishamtembelea majeruhi katika hospitali ya Muhimbili alikolazwa

TCRA YATAMBUA RASMI MCHANGO WA MITANDAO YA KIJAMII (BLOGS),WAZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA MATUMIZI MAZURI YA MITANDAO YA KIJAMII.



Msanii wa muziki wa asili Tanzania ambaye pia ni msanii wa maigizo na filamu, Mrisho Mpoto akizungumza jambo mbele ya waaandishi wa habari na wamiliki wa blogs mbalimbali katika uzinduzi wa matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii. Mrisho alisimama kuzungumza dakika chache baada ya wimbo alioimba na Banana Zoro kuzinduliwa, unaojulikana kama 'Futa, Delete Kabisa'. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),John Nkomo katika uzinduzi huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkomo, akizungumza mbele ya wamiliki wa blogs mbalimbali Tanzania, waandishi wa habari katika warsha ya kampeni ya kuzindua matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuhamasisha suala zima la maendeleo.


Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), waandishi mbalimbali wa habari pamoja na wamiliki wa mitandao ya kijamii, Blogs, wakisikiliza maneno mazuri kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Tanzania, Profesa John Nkomo, hayupo pichani. Hii ni sehemu maalumu ya kuonyesha kuwa TCRA wanatambua mchango wa mitandao ya kijamii, hususan blogs na wamiliki wao kwa ujumla.

Afisa Uhusiano wa TCRA,Innocent Mungi akiwakaribisha wadau mbalimbali wa mambo ya habari za kwenye mitandao,kuhusiana na uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano,Warsha hiyo imefanyika leo Makao makuu ya Ofisi hizo,zilizopo barabara ya Sam Nujoma jijini Dar.

Wadau wa mawasiliano wa mitandao ya kijamii, blogs, wakisikiliza hoja mbalimbali zilizotolewa na viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA katika uzinduzi wao wa matumizi mazuri ya mitandao kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo ya Taifa.
Habari kamili inakuja

WAASI WA M23 WAPEWA MASAA 48 YA KUSALIMISHA SILAHA ZAO.....VINGINEVYO NI BALAA TUPU



Wanajeshi wa Brigedi Maalum wakiwa katika mazoezi makali yaliyofanyika hivi karibuni huko Goma Mashariki ya Demokrasia ya Kongo..

Mmoja wa walinda amani kupitia Brigedi Maalum inayoundwa na wanajeshi kutoka Tanzania, Afrika ya Kusini na Malawi akiwa katika moja ya mazoezi yaliyofanyika hivi karibu huko Goma.

Kamanda Mkuu wa Misheni ya Kulinda Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ( MONUSCO ) Luteni Jenerali Carlos Albeto dos Santos Cruz ametakanza jana jumanne akiwa Goma kwamba MONUSCO itaanza rasmi kuitumia Brigedi Maalum na ametoa saa 48 kuanzia saa kumi jioni kwa saa za Goma jana siku ya Jumanne waasi wote kusalimisha silaha zao, na kwamba ifikapo saa kumi jioni kwa saa za Goma siku ya Alhamisi Agosti Mosi wale wote ambao watakuwa hawajasalimisha silaha zao watachukuliwa kama tishio la usalama kwa wananchi na MONUSCO italazimika kuwapokonya ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu kwa mujibu wa Mamlaka iliyopewa na Sheria zinazowaruhusu kufanya hivyo.
------------------------------
Misheni ya Kutuliza Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( MONUSCO) imetangaza kwamba kwa mara ya kwanza itaanza kuitumia Brigedi Maalum ( Force Intervention Brigade) katika kudhibiti eneo maalum la usalama ( security zone ) kuzunguka mji wa Goma ulioko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na imewapa saa 48 waasi kusalimisha silaha zao.

Taarifa iliyotolewa na MONUSCO na kusambazwa na Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa jana jumanne, inaeleza kwamba watu binafsi katika eneo la Kivu ya Magharibi ambalo linajumisha Goma na Sake na ambao hawahusiki na vyombo vya usalama watapewa saa 48 kuanzia saa kumi jana kwa saa za Goma ( Jumanne ) kuzisalimisha silaha zao katika Misheni hiyo na kujiunga na mchakato wa DDR/RR unaoratibu upokonyaji, usambaratishaji, urejeshwaji makwao, kuwaunganisha na jamii na kuwapatia makazi.

Baada ya saa kumi jioni ya Alhamisi, Agosti Mosi. Taarifa hiyo inasema. Wale wote ambao watakuwa hawajasalimisha silaha zao watachukuliwa kama tishio kwa usalama wa wananchi na MONUSCO itachukua hatua zote muhimu kuwapokonya silaha hizo ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu kama ilivyoainishwa katika Mamlaka na sheria za ushiriki za MONOSCO.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo zaidi ya wananchi milioni moja wanaishi katika eneo dogo la Goma na Sake na kando kando ya barabara ambayo inawaunganisha na kambi ya wakimbizi ya Mugungu ambayo ni makazi ya muda ya watu karibu 70, 000 ambao wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano.

Kwa mujibu wa MONUSCO, tangu kati kati ya mwezi Mei eneo hilo limeshuhudia mapigano ya mara kwa mara kutoka kwa kundi la M23 dhidi ya majeshi ya Serikali ya FARDC ikiwa ni jaribio la wazi la kutaka kusonga mbele kuelekea Goma na Sake.

“ Katika mashambulizi hayo, likiwamo la hivi karibuni la Julai 14, M23 walitumia kiholela silaha zao za moto zikiwamo silaha nzito ambazo zimesababisha wananchi kujeruhiwa” .

Taarifa hiyo imeongeza kwamba kundi hilo la M23 katika mashambulizi hayo limelenga pia Vituo vya Umoja wa Mataifa.

Aidha taarifa hiyo inabainisha kwamba eneo hilo maalum la usalama ( security zone) litasaidia kudhibiti tishio la moja kwa moja mbali na eneo la nje ya Goma na pengine eneo hilo linaweza kupanuliwa na kurudiwa sehemu nyingine kutakako hitajika.

Tamko hilo la kutoa saa 48 kwa waasi kusalimisha silaha zao linafuatia kuwasili katika eneo la Goma kwa Kamanda Mkuu wa MONUSCO, Luteni Jenerali Carlos Alberto dos Santos Cruz, ambaye alitangaza kwamba Misheni ya MONUSCO itaunga mkono jeshi la Serikali ( FARDC) katika kuanzisha eneo la usalama kuzunguma eneo la Goma na vitongoji vyake.

Taarifa hiyo inamkariri Kamanda Mkuu wa MONUSCO akiyapongeza majeshi ya serikali kwa kazi nzuri iliyofanya wiki iliyopita ya kuwadhibiti M23. Ingawa anasema eneo la Goma na Sake bado limo katika mazingira magumu sana na kwamba ni wajibu wa wahusika wote kuhakikisha wahalifu wote hawaendelei kuhatarisha raia wa eneo hilo.

Kwa mwaka uliopitia , kundi la M23 pamoja na makundi mengine yenye silaha yamekuwa yakipambana mara kwa mara na majeshi ya serikali katika Mashariki ya Kongo, huku makundi hayo yenye silaha mwezi Novemba mwaka jana yakiikalia Goma kwa muda.

Aidha mapingano ya hivi karibuni ambayo safari hii yalihusisha pia kundi jingine la wanagambo wenye silaha lenye asili yake nchini Uganda, yamesababisha zaidi ya wananchi 100,000 kuyakimbia makazi yao na hivyo kuongeza mgogoro wa kibinadamu katika eneo hilo linalohusisha watu wengine 2.6 milioni ambao wameyakimbia makazi yao huku wengine 6.4 milioni wakihitaji chakula na huduma za dharura.

Wakati huo huo, Kaimu Mkuu wa MONUSCO Bw. Moustapha Soumare katika taarifa yake ametoa wito kwa pande zote kutafuta suluhu ya kisiasa kwa matatizo ya DRC kupitia Mpango Mpana wa Kisiasa wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani, usalama na ushirikiano wa maendeleo katika DRC na eneo la Maziwa Makuu uliopitisha mwezi wa Februari na viongozi 11 wa Afrika na Taasisi nne za Kikanda na Kimataifa.
Aidha akasema katika kipindi hiki ambacho suluhu la kisiasa linatafutwa MONUSCO itatumia nguvu iliyonayo kuwalinda wananchi dhidi ya hatari zitokanazo na makundi ya waasi.

MONALISA AGOMA KUOLEWA TENA BAADA YA KUACHIKA MARA KADHAA.



Msanii mkongwe kwenye soko la filamu Tanzania,Yvonne Cherry "Monalisa" amesema hatarajii kuolewa tena baada ya kuvunjika kwa ndoa zake kadhaa ikiwemo ile ya producer Tyson....
Akisimulia mikasa ya maisha yake mbele ya mwandishi wetu,Monalisa aliema kuna siku walipokuwa kwenye kikao cha sendoff ya mama yake, alitania na kusema ataolewa disemba lakini hakuwa serious....

"Sina mpango wa kuolewa kabisa,kwanza sina mchumba, ntaolewaje?

"Siku ile nilikuwa natania tu kwa sababu sipo tayari kuolewa na kuachika tena"..Alisema Monalisa

ROSE NDAUKA ANASWA AKIPAPASWA NDANI YA GARI KABLA YA KUPELEKWA HOTELINI



Rose Ndauka au Aisha anaweza kuwa ameitia najisi funga yake baada ya kunaswa akiingia hotel moja iliyoko kinondoni jijini Dar kwa kile kilichoelezwa ni kwenda kuivunja amri ya sita na mwanamziki wa bongo fleva Nassoro Ayoub "Nasry" au Tajiri Boy

Rose ambaye alisilimu mwaka jana na kupewa jina la Aisha baada ya kuchumbiwa na mwanamziki mwasisi wa kundi wa TNG Squad, Malik Bandawe, alifumwa na kamera za wakazi wa jirani na hoteli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.....

Shuhuda wa tukio hilo amedai kwamba majira ya mchana kweupe gari aina ya Toyota Mark X lenye rangi nyeusi liliwasili kwenye viunga vya hoteli hiyo na kusimama kwa takribani dakika 10 kisha likaondoka na kwenda kupaki sehemu nyingine ambapo ni umbali mfupi toka hotelini hapo...

Kitendo hicho kiliibua mashaka miongoni mwa watu hasa kutokana na vioo vya gari hilo kuwa tinted hivyo kutowaonesha waliokuwemo ndani...

"Walipoondoka na kupaki palipojificha tuliamua kuwasogelea ili tujue ni akina nani

"Baada ya muda, kioo cha dereva kilishushwa kidogo, tukamuona dogo anayefanana na Diamond akiwa anampapasa demu aliyekuwa pembeni yake...

"Tulipoona hivyo, tulidhana mnyamwezi ameamua kumaliza mambo yake ndani ya gari, hivyo tukaziweka simu zetu standby kwa ajili ya kushuhudia" alisema shuhuda huyo

Baada ya muda, mlango wa kulia ulifunguliwa kisha wakamuona dogo aliyetambuliwa kwa jina la Nasry

"Kumbe hakuwa Diamond,alikuwa ni dogo Nasry.Tulipotupa jicho ndani, tulihamaki kumuona Rose Ndauka akibadili nguo na kujitanda baibui.

"Nadhani alifanya hivyo ili watu wasimjue pindi atakaposhuka kwenye gari maana aliposhuka tu, waliongozana na dogo Nasry kwa mwendo wa kasi hadi ndani...


"Toka walipoingia ndani hadi walipotoka iliwachukua kama masaa matatu hivi.Wakati wa kutoka, Nasry alilifuata gari hadi mlangoni na kisha Rose akaingia na kutokomea"...Kilimalizia kusimulia chanzo hicho

Tuesday, July 30, 2013

KESI YA LADY JAYDEE YAPIGWA KALENDA


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, leo ililetwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na wakili anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na kumtuma mwakilishi wake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama Kuu kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo.
Kwa mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia mitandao ya kijamii.

FEZA AONGOZA KUCHUKIWA NA WENZAKE NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER


Habari mbaya kwa Tanzania, Feza Kessy ni miongoni mwa washiriki watatu waliopigiwa kura zaidi kutoka wiki hii...FEZA amepata kura nyingi zaidi hii inaonyesha kuwa ndio mshiriki anayechukiwa zaidi ndani ya jumba hilo...
Feza ameungana na mpenzi wake Oneal na Elikem kwenye kikaango hicho cha eviction. Wa kwanza kumtaja Feza kwa kudai kuwa ni mbeya na jinsi anavyopenda kuwakusanya washiriki wenzake na kuwashawishi mi Msouth, Angelo.

Beverly wa Nigeria pia amemtaja Feza kwa madai kuwa ana upinzani mkali kwenye shindano hilo.

Elikem amewataja Oneal na Feza huku Cleo wa Zambia akimtaja Feza kwa madai kuwa ni tishio kubwa kwake na kusema wazi kuwa hataki kumuona Feza anaondoka na dola laki tatu.

Haya sasa muda wa kuanza kumpigia kura Feza Kessy asitoke ndio huu.

WAKUTWA NA MAUTI WAKIFANYA MAPENZI.


. Kwa Mujibu wa Ripoti iliyotolewa na wakazi wa eneo husika, inasemekana kwamba Bw. Mathias Nwoko,45, na Binamu yake Angela Ihuoma walifikwa na Umauti wakati wakiwa katika tendo la ndoa.
Wawili hao ambao asubuhi kabla ya kufariki walionekana pamoja wakicheza kwa furaha katika sherehe za kumkaribisha Padri Mpya katika Jimbo lao, Mathias ambaye ameelezwa alikuwa ndani ya ndoa kwa kipindi cha miaka 13 bila ya kupata mtoto alirudi na binamu yake usiku wakitokea kusikojulikana na kumkuta mkewe akiwa anaangalia T.V nyumbani kwake.
Mathias alimwambia mkewe atangulie kulala kwasababu yeye anachukua tochi amsindikize binamu yake huyo kwao. Mama mzazi wa Angela alipoona usiku unazidi na mwanawe hajarudi alimtafuta kupitia simu yake ya mkononi ambayo alipokelewa na Mathias akimwambia wapo pamoja.
Mpaka asubuhi, Si Mathias wala Angela Aliyerudi kwao na ndipo familia zote mbili zilipoingiwa na wasiwasi, Mke wa Mathias alienda katika nyumba yao ya pembeni asubuhi hiyo na ndipo alipowakuta wawili hao, mwanamke akiwa juu ya mwanaume.
Aliganda kwa muda asiamini anachokiona,hasa kuona wawili hao hawashtuki japo kawaona na ndipo alipogundua ya kwamba wamefariki Dunia. Ilibidi kutoa taarifa kwa familia ya Angela ambapo alikuja mama yake mzazi ambaye alipigwa na butwaa kutokana na picha iliyokuwa mbele yake.
Miili yao ilitenganiswa na kupelekwa hospitali huko Ogbor Nguru, jimbo la Aboh Mbaise.

"WAPIGWE TU" YA MIZENGO PINDA KUMFIKISHA KORTINI



KAULI ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ya kubariki vyombo vya dola kuendeleza kipigo kwa raia wanaokaidi amri imechukua sura mpya baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Bindamu (LHRC) kutangaza kumburuza mahakamani wiki hii kutokana na kushindwa kufuta kauli yake.

Juni 20, mwaka huu, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo bungeni, Waziri Mkuu, Pinda, alivitaka vyombo vya dola kuendelea kuwapiga raia, akisema kuwa hakuna namna nyingine kwani serikali imechoka.

Kauli hiyo imekuwa ikipingwa na wananchi, mashirika ya kutetea haki za binadamu na wanasiasa wakimtaka Waziri Mkuu, Pinda, kuifuta kwa kuomba radhi, wakidai kuwa inachochea uvunjifu wa sheria.

Akitangaza kusudio la kituo hicho kufungua kesi dhidi ya Pinda, Mkurugenzi wa maboresho na utetezi, Harold Sungusia, alisema hadi jana walikuwa tayari wameandaa kusudio la shtaka lao.
Alisema kuwa kisheria kilichowafanya kufikia uamuzi huo ni kutokana na waziri mkuu huyo kukiuka Katiba ya nchi inayozungumzia usawa mbele ya sheria.

“Kitendo alichofanya waziri mkuu cha kuwaruhusu polisi kupiga wananchi hakikubaliki hata kidogo na walitegemea kwamba angeomba radhi kutokana na kauli yake hiyo tangu alivyoshinikizwa kufanya hivyo na makundi mbalimbali.
“Badala yake ameendelea kuwa kimya licha ya mkubwa wake, Rais Jakaya Kikwete, hivi karibuni kukiri kwamba mtendaji wake huyo aliteleza,” alisema.

Sungusia aliongeza kuwa Alhamisi wiki hii wataweka bayana kwa waandishi wa habari ni wapi kesi hiyo itafunguliwa.

Pinda alitoa kauli hiyo tata ambayo imehojiwa na wengi wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM) aliyehoji kama serikali iko tayari kutoa tamko kuhusu vurugu zilizotokea jijini Arusha, Mtwara na maeneo mengine pamoja na hatua ya vyombo vya dola kutumia nguvu.

Katika majibu yake Pinda alisema kuwa suala la amani linawagusa wote, kwamba jukumu ni kwa viongozi wa kisiasa. Alifafanua kuwa kama viongozi wa kisiasa hawatafika mahali wakakubaliana bila kujali vyama vyao nchi itafika pabaya.

Pinda alifafanua kuwa kwa upande wa serikali lazima wahakikishe kwamba wale wote wanaojaribu kuvunja amani kwa namna yoyote ile kazi waliyonayo ni kupambana kweli kweli kwa njia zozote zinazostahili.

“Mimi naomba sana Watanzania, maana kila juhudi zinazoonekana zinaelekea huko, tunapata watu wengine wanajitokeza kuwa mara unajua…unajua. Acheni serikali itimize wajibu wake, kwa sababu jambo hili ni la msingi na wote tulilinde kwa nguvu zetu zote.

“Mheshimiwa Mangungu umeanza vizuri lakini hapa unasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo unaambiwa usifanye hiki, ukaamua wewe kukaidi, utapigwa tu,” alisema.

Waziri mkuu aliongeza kuwa hakuna namna nyingine, maana lazima watu wakubaliane na serikali kwamba nchi hii wanaiendesha kwa misingi ya kisheria.

“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ni jeuri zaidi, watakupiga tu, na mimi nasema wapigwe tu, maana hakuna namna nyingine, tumechoka,” alisema

Monday, July 29, 2013

JACK WOLPER AMJIBU MBAYA WAKE ALIYETANGAZA KUWA YEYE NI KAHABA


Msanii nyota wa filamu bongo, Jacqueline Wolper amewataka wasanii wa bongo movie kuacha tabia ya kupigana majungu ya kinafiki ambayo huchangia kujenga bifu za kijinga....

Akiongea na mpekuzi wetu, wolper alidai kuwa kuna mipaka ya watu kuishi lakini kuna baadhi ya wasanii wanaamini kwamba majungu ndo mshahara wao kiasi kwamba wasipomsengenya mtu basi hawawezi kuishi...

Wolper anadai kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii wanaosemwa sana kwa mabaya hasa kuhusu maisha yake ya kila siku.Hali hiyo inatokana na umaarufu alionao ambao huwafanya wasanii wenzake wamchukie hasa wasanii wa kike...

Hii ni kauli ya Wolper alipoongea na ripota wetu:

"Wasanii tungekuwa na ushirikiano kama nisha tungefika mbali sana.

"Mimi simuogopi mtu katika maisha yangu, lakini ninachohitaji katika maisha yangu ni Heshima.

"Ukiona nimekukwaza, basi njoo nyumbani au nambie nikufuate ili tuyamalize kibinadamu na si kudhalilishana mitandaoni...


"Kuna msanii mmoja wa kike amekuwa akinichafua sana mitandaoni kwa kuniita kahaba, najuza na matusi mengine kibao.

"Huyo ni mtu anayetafuta pakutokea, anatafuta kujulikana kupitia Wolper na pengine kafulia na sasa anatafuta mtaji.

"Tangu anitukane sikuona haja ya kumjibu kutokana na heshima niliyo nayo katika kazi yangu na heshima yangu kwa wazazi , ndugu na jamaa.


"Niliamua kumwachia mungu.Kama ni kahaba au najiuza, mungu anajua.Alisema Wolper

MSHIRIKI WA TANZANIA (NANDO ) ATIMULIWA BIG BROTHER BAADA YA KUGOMBANA NA MSHIRIKI MWENZAKE



Jana usiku mara tu baada ya Sulu na Annabel kutolewa kwa kura za watazamaji, Big Brother aliwaita washiriki pamoja katika kikao cha dharura kufuatia ugomvi uliotokea kati ya Nando na Elikem.

Itakumbukwa kwamba siku ya ijumaa ilitokea hali ya kutoelewana kati ya Nando na Elikem. Wawili hawa walitukanana sana na kutishiana mno. Ugomvi huo ulianzishwa na Nando.

Kwa mujibu wa sheria za Big Brother mwaka huu, kuanzisha ugomvi ni kosa ambalo hupelekea kupata 'strike' ama onyo.

3 strike rule ni mtindo unaotumika msimu huu. Kwa mujibu wa Big brother, yeyote atakaye fanya makosa matatu makubwa na kupewa maonyo matatu basi moja kwa moja anatakiwa atimuliwe..

Sheria hiyo imetumika kumtimua Nando kwa sababu 1. Alianzisha ugomvi siku ya Ijumaa, 2. Alishiriki ugomvi na Elikem na 3. Alitishia maisha, "I feel like stabbing him. A nigga like that deserves to die"...

Katika kipindi cha wiki 9 za ushiriki wake katika jumba hilo, Nando amekutwa na misuko suko kadhaa ikiwemo kuwahi kukutwa na kisu katika Party ya Channel O pia kukutwa na mkasi chini ya kitanda kitu ambacho ni kinyume cha sheria za big brother.

Kutokana na ugomvi huo Elikem alipata strike moja.

Big brother alimtaka Nando aondoke katika jumba lake hilo na kutumia fursa hiyo kuwataka washiriki wengine waishi kama watu wazima.

"SIJAWAHI PIGA PICHA ZA UCHI...NIMEMFAHAMU SINTAH KUPITIA SKENDO YA KUGAWA PENZI KWA NATURE"...RAYUU AFUNGUKA TENA



Jana, Bongomovies.com imefanya interview kwa njia ya simu na mwanadada msanii Rayuu alaice Bungenzi kuhusiana na mambo mablimbali yanayoandikwa kwenye mitandao na tovuti mbalimbali nchini.

Katika interview hiyo waliweza kupata mambo manne kama ifuatavyo:

1. Hajawai kupiga picha za utupu na kuzisambaza ili kupata umaarufu


Akiongea kwa msisitizo Rayuu amesema kuwa hajawai kupiga picha za utupu na kuzisambaza kwenye mtandao kwa ajili ya kupata umaarufu.


“Sijawai kusambaza picha za utupu ili nipate umaarufu, hizo picha kweli ni zangu na ukizitazama vizuri sio picha za utupu kama watu wanavyosema(?????), ni picha nilizopiga kwenye simu yangu kujiangalia tattoo yangu niliyochora kiunoni lakini kuna marafiki zangu waliochukua simu yangu na sijui ni nani ndio zilisambaa kutokea hapo na kila mtu kuandika stori anayoijua yeye” Alisema.

2. Hafahamiani na wala hajawai kuonana na sintah kwa zaidi ya miaka mingi sana


Rayuu amesema kuwa hajawai kuonana na sintah, wala hafahamiani naye personally na huwa anashangaa sana kwanini mwanadada huyu anamchafua kwenye blog yake.

“Kiukweli mi sifahamiani na Sintah, na wala hatujawahi kuonana kwa kipindi kirefu sana, sasa huwa nashangaa kwanini ananichafua na kunitukana kwenye blog yake. Kuna kipindi nilichoka nikaanza kumjibu lakini baadaye nikaona ni utoto bora ninyamaze kwanza nione kama ataacha lakini nashangaa hakui.

Huyu dada mi huwa simuelewi kwakweli,anagombana na kila mtu, nahisi anaweza kugombana hata na panya. Kwanza ni mtu mzima sana kwangu.

Nakumbuka mi nimemfahamu yeye wakati teyari kashakuwa maarufu na skendo za uroda kwa Juma nature na mimi nilikuwa bado mdogo sana. Sa sijui kwanini hakui. Kila siku anatukanwa kwenye blog yake lakini wala hajali.”…Alisema Rayuu

3. Marehemu Mzee Kipara ndiye haswa aliyemuingiza kwenye sanaa
Watu wengi hawajui kuwa marehemu mzee kipara ndiye aliyemuingiza Rayuu kwenye sanaa. Rayuu alisema kuwa anakumbuka siku moja kundi la kaole walienda kurekodi igizo lao mitaa ya nyumbani kwa kina Rayuu na alipowaona alimfuata mzee kipara na kumueleza nia yake na ndipo alipompeleka na kumtambulisha kwenye kundi la kaole na kuanza kupata nafasi ya kuigiza na kufanya mazoezi kundini hapo.
4. Sio mtu wa kutoka sana na akila "bata" anaumwa sana kesho yake

Rayuu amesema yeye sio mtu wa kutoka na kupenda kwenda club kama wengi wanavyodhani bali hupenda sana kushinda ndani kwani akifanya hivyo kesho yake lazima aumwe siku nzima

-bongomovies.com

"SASA NIMEOKOKA.....UJINGA SITAKI TENA"...LULU MICHAEL



MUIGIZAJI machachari wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema baada ya kupata misukosuko ya kimaisha, sasa maisha yake ameyaelekeza katika sala kumuomba Mungu amsamehe makosa yake.

Lulu alisema hayo juzi, katika kipindi cha Friday Night Live (FNL), kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha EATV cha Jijini Dar es Salaam.

“Sasa hivi nasali sana, namuamini Mungu katika maisha yangu na mbali ya kwenda kanisani, pia nasali mwenyewe katika sala zangu.

“Ningependa maisha ya sasa ninayoishi ningeishi siku za nyuma, lakini yote ya Mungu labda maisha yale nisingeyaishi siku za nyuma, ningekuja kuyaishi baadaye,” alisema Lulu.

Katika hatua nyingine, alisema anavutiwa na kazi ya msanii wa bongo fleva, Bernard Paul ’Ben Pol’ ambaye tungo za nyimbo zake zinamkosha kuzisikiliza.

"NIKIKUTA NINA VIRUSI VYA UKIMWI NI LAZIMA NIJIUE MAANA SIPO TAYARI KUCHEKWA".....BABY MADAHA


Msanii wa filamu bongo,Baby Madaha amefunguka kwamba siku akianza kuona dalili za ugonjwa wa UKIMWI ndani ya mwili wake atakunywa sumu kwa kuhofia kuchekwa na jamii..

Akiongea na mwandishi wetu,Madaha amedai kuwa kwa sasa anaamini hana ngoma maana siku zote hutumia Kinga (kondom) ili asiambikizwe gonjwa hilo japo hana uhakika asilimia zote maana hiyo ni mipango ya mungu.

"Siukatai ugonjwa huo kwa kuwa sijui ni lini naweza kuupata hasa ukizingatia kwamba mimi bado ni kijana mbichi ambaye bado nahitaji kuifurahia dunia"...Alisema Baby Madaha..

Katika mazungumzo hayo, Madaha anadai kwamba mpaka sasa hakuna mpenzi wake yeyote aliyekufa kwa Ngoma ingawa wapo waliofariki kwa maradhi ya kawaida na ajali....

"Nikijua tu nina ngoma ni lazima ninywe sumu ili kukwepa balaa la wabongo.Najitahidi kujilinda ili nisiudake mapema"..Alisema Madaha

Madaha anadai kwamba kitendo cha yeye kujiua mapema kitasaidia kuwaondolea wasiwasi wasanii wenzake ambao wataanza kujiuliza maswali mengi kuhusu watu aliowahi kutoka nao kimapenzi

"Nitawasaidia wasanii wengine ambao nimewahi changia nao mabwana.Najua wataumia sana, lakini ndo hivyo tena, hakutakuwa na jinsi.

"Sijasema nina UKIMWI,Hapana,nimesema kwamba ikitokea maana watu hawakawii kupindisha maneno"..Madaha

DK SLAA AMWEKA KITIMOTO NCHIMBI-ZUIA UHALIFU SIO UPINZANI


 
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi jana alikuwa na wakati mgumu katika Kongamano la Amani lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa kumtaka ajiuzulu kutokana na kushindwa kudhibiti uhalifu nchini.
Mbali ya Dk Nchimbi, Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi katika kongamano hilo, Brigedia Jenerali, Elias Athanas naye alibanwa akitakiwa kueleza tuhuma za askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kuhusishwa na vitendo vya ubakaji na utesaji wa raia mjini Mtwara.
Akizungumza katika kongamano hilo, Dk Slaa alisema hakuna haja ya kutafuta mchawi wa amani ya nchi bali, Serikali inapaswa kulaumiwa kutokana na watendaji wake kushindwa kuwajibika ipasavyo.
Alitoa mfano wa kitendo cha Bandari ya Dar es Salaam kutumiwa kupitisha pembe za ndovu wakati maofisa polisi wakiwemo ni kitendo cha aibu ambacho kinatosha kumfanya Waziri Nchimbi ajiuzulu.
Akijibu madai hayo wakati akihitimisha kongamano hilo, Waziri Nchimbi alikiri kuwa baadhi ya polisi wamekuwa na tabia ya kujihusisha na rushwa na katika kupambana na hali hiyo, Serikali imeshawatimu kazi askari 101 katika kipindi cha mwaka 2012.
Hata hivyo, Dk Nchimbi alisema suluhisho la matatizo yaliyopo ndani ya Jeshi la Polisi siyo kuwatimua kazi askari pekee na ndiyo maana Serikali imeanza mkakati wa kutoa mafunzo ya maadili ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa weledi.
Alisema ataendelea kupokea changamoto kutoka kwa wadau wote wa amani na kupongeza waliobuni kongamano hilo, huku akiahidi kutoa ushirikiano kufanikisha jambo lolote linalohusiana na mjadala wa amani ya nchi.
Kuhusu ubakaji na utesaji wa wanajeshi, Dk Slaa alisema inasikitisha kuona jeshi ambalo linapaswa kulinda amani linatesa na kuwabaka raia.
Kauli hiyo iliungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro ambaye alisema anao ushahidi wa wanachama wa chama chake waliojeruhiwa na kupakwa pilipili akisema kwamba jeshi hilo limekuwa na baadhi ya askari wakatili tofauti na misingi ya kuanzishwa kwake.
Akijibu tuhuma hizo, Brigedia Jenerali Athanas alikanusha madai hayo akisema siyo kweli kwamba JWTZ linaendesha unyama na kwamba lipo Mtwara kwa ajili ya kulinda amani na kusema tuhuma hizo ni za mitaani.
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alidai kuwa tangu nchi ilipopata uhuru haijawahi kuwa na amani ya kweli akitoa mfano wa wananchi kuhamishwa kwa nguvu katika maeneo yao.
Alisema katika siku za karibuni, tofauti na zamani polisi ilipokuwa ikifanya kazi ya kudhibiti uhalifu, sasa inaonekana kama kazi yake ni kudhibiti upinzani na limekuwa likituhumiwa mara kwa mara kwa kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani na kusababisha mauaji.
Alipiga kijembe akisema kwamba CCM kinakaribia kuanguka na ndiyo maana kimekuwa kikitumia mabavu kudhibiti upinzani.
Awali, Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Gaudence Mpangala alisema amani inaweza kutoweka ikiwa CCM kitaendelea kutumia dola kudhibiti upinzani.
Alisema CCM kinapaswa kufanya kazi kama ilivyo vyama vingine vya siasa na kuonya kwamba hata kukiwa na makongamano mengi, amani haitapatikana kama hakitajitathmini na kuchukua hatua.
Alisema polisi imekuwa ikifanya makosa kuzuia maandamano ya vyama vya upinzani akisema sheria iko wazi ikisema vinachotakiwa kufanya ni kulitaarifu jeshi hilo kuhusu ratiba ya shughuli zake.

MASOGANGE BALAA JIPYA,MAHAKAMA YAMFUTIA DHAMANA ARUDISHWA LUPANGO



 HUKU akiwa hajui nini hatima ya kesi inayomkabili ya kunaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini, Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’ amepata balaa jipya,GUMZO LA JIJI lina taarifa kamili... 
Dawa za kulevya. Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo nchini humo, Masogange na mwenzake aliyekamatwa naye, Melisa Edward wamefutiwa dhamana hivyo wamerudi tena rumande.


Agnes Gerald ‘Masogange’. KWA NINI DHAMANA IFUTWE?
Habari zinadai kuwa, dhamana za wawili hao zimefutwa kufuatia kuhisiwa kwamba wana mpango wa kuondoka nchini huko kinyemela na kurejea Tanzania, jambo ambalo limetafsiriwa kama jaribio la kuikimbia kesi hiyo.
“Unajua huku Sauzi si kila mtu anawaonea huruma Masogange na Melisa kwa tatizo lililowapata, sasa utakuta maskani mtu anaropoka vitu vya ajabu pengine vya uongo bila kujua kuwa si kila mtu anayesikiliza atayaachia hapohapo, wengine ni ‘mainfoma’ wanayafikisha mbele.

“Hicho ndicho kilichomtokea Masogange, wakati baadhi ya watu wakiwa kwenye mchakato wa kumsaidia ili kujua jinsi gani kesi yake itakwenda haraka, wengine wanakwenda kuongea mambo ya ajabu kwa watu wao wanaowatuma kuwapelekea taarifa, eti kuna watu wanajipanga kuwatorosha, si sheria ikafuata mkondo wake.
“Hii inatupa wakati mgumu sisi tuliokuwa tumsaidie, mara kwa mara tunaitwa na kuhojiwa na jeshi la polisi. Ndiyo maana dhamana yao imefungwa, ukiangalia nini kilichosababisha ni maneno ya uongo yanayotokea maskani,” kilisema chanzo hicho ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake.
MASOGANGE AKAUKA MITANDAONI
Licha ya kukumbana na kesi ya madawa ya kulevya, Masogange aliendelea kutumbukiza picha zake kwenye mitandao ya kijamii na kuzielezea, lakini baada ya kufutiwa dhamana amekauka mitandaoni kwa picha za karibuni.
“Nyiye si mnaona, siku hizi haposti tena picha zake mpya kama palepale katikati baada ya kukamatwa. Siku zile alikuwa nje kwa dhamana, sasa yupo rumande hawawezi kumwachia akacheza na simu,” kilisema chanzo.
WABONGO WALIOJITOLEA FEDHA KUMWOKOA WASIKITIKA
Baada ya staa huyo kutiwa nguvuni Julai 5, mwaka huu, baadhi ya Watanzania waishio Bongo na kule Afrika Kusini walidaiwa kuchanga fedha kwa lengo la kumsaidia mrembo huyo lakini kufuatia kuvuja kwa taarifa za kufungwa kwa dhamana yake, wamekosa nguvu na kusikitikia kitendo hicho.
 
Kamanda Nzowa.
SHERIA ZA AFRIKA KUSINI NA TANZANIA KUHUSU ‘UNGA’ SI SAWA?
Inadaiwa kuwa, nchini Afrika Kusini mtu akikamatwa na ‘unga’ anaweza kuwa nje kwa dhamana wakati kesi yake ikiendelea kusikilizwa mahakamani, Tanzania mtu akinaswa na unga kesi inasikilizwa akiwa rumande.
POLISI HAWAKAUKI NYUMBANI KWAKE
Habari kutoka vyanzo vya hapa Bongo zinadai kuwa, askari polisi (kituo cha kazi hakijajulikana) wamekuwa wakifika nyumbani kwa msanii huyo, Kijitonyama, Dar na kuwauliza mambo kadhaa majirani.
“Jamani ishu ya Masogange vipi? Maana hapa mtaani kuna polisi wamekuwa wakija mara kwa mara na kumuulizia kama yupo. Wao hawajitambulishi kama askari lakini watatu kati yao wamebainika ni polisi,” kilisema chanzo hicho.
Kiliendelea kudai kuwa, Julai 20, mwaka huu alifika askari mmoja na kuuliza majirani kama wamewahi kumwona mwanaume mrefu, mweupe akiingia kwenye nyumba ya Masogange.
“Julai 20 alikuja afande mmoja, akawauliza majirani kama kuna siku yoyote ambayo mwanaume mrefu, mweupe aliingia kwa Masogange, akajibiwa hajawahi kufika mtu wa aina hiyo.
“Ndiyo maana nikauliza kesi yake vipi kule Bondeni (Afrika Kusini)? Ila kuna kitu nilikisikia kwa baadhi ya watu kwamba kuna ndugu yake atakuja kuhamisha vyombo vyake kwa sababu wanajua kesi itachukua muda mrefu,” kilisema chanzo.

Masogange. KUMBUKUMBU
Julai 5, mwaka huu, Masogange na Melisa walinaswa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo mjini Kempton Park, Afrika Kusini.
Ilidaiwa kuwa thamani ya mzigo huo wenye kilo mia moja na hamsini ni shilingi bilioni moja na laki sita...

Saturday, July 27, 2013

RAY C ATANGAZA KURUDI UPYA KWENYE GAME LA MUZIKI


Mabibi na mabwana mko tayari kwa ujio mwingine wa Ray- C. Malkia wa kiuno bila mfupa Rehema Chalamila aka Ray-C ametangaza ujio wake rasmi baada ya kuwa chimbo kwa kipindi kirefu toka apate matatizo miezi kadhaa iliyopita. Ni baada ya siku chache kupita toka Ray-C atamke kuwa anapenda sauti ya ‘dogo lake’ Recho na kuwa atakuja kufanya naye kazi, leo amethibitisha kuwa mwezi Agosti ndio anarudi rasmi kutoka chimboni.

Kupitia akaunti ya Instagram Ray-C aliweka picha ya gazeti moja lililoandika ‘Ray-C kuonekana hadharani mwezi Agosti’, na baada ya followers wake kutaka ufafanuzi ndipo alifunguka kwa kusema “For Sure it’s bout time nw nimewapa muda sana watoto sasa mdada is coming back”.

Ray C aliwauliza marafiki zake wa Instagram kama wapo tayari kwa ‘come back’ yake, wengi wameonekana kutamani muda ufike waweze kumuona tena Ray-C akirudi katika muziki. Hizi ni baadhi ya comments kutoka kwa mashabiki wake.

HABARI KUHUSU ALLY KIBA KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA AMSTERDAM


Siku hizi Tanzania kumekua na mambo meeeengi yanayozushwa au kuanzia kwenye mitandao ya kijamii sanasana facebook na twitter ambapo miongoni mwa makubwa ya wiki hii ni stori kwamba mwimbaji wa Bongofleva Ally Kiba amekamatwa na polisi wa Amsterdam kwa tuhuma mbalimbali na wengine walidiriki kuripoti kwamba ni dawa za kulevya.Ally Kiba mwenyewe aliandika kwenye page yake ya twitter kama kukanusha lakini ni tweet ambayo haikuwa rahisi kuielewa au kufahamu alichomaanisha kama unavyoona hapa chini..

Baada ya hii tweet ilibidi millardayo.com imuendee inbox au DM kumuuliza kama ni kweli alikamatwa ambapo hili ndio jibu lake….


Huenda siku kadhaa zijazo Tanzania ikapata sheria mpya itakayokua inadili na watu wanaoitumia vibaya mitandao kama vile kutukana, kuandika uongo na mengine kama hayo… July 26 2013 Wakili Mwandamizi wa Serikali alisema makosa ya kwenye Internet yameongezeka sana Tanzania na hakuna sheria inayodili nayo moja kwa moja hivyo kuna mpango wa kuipata sheria ya hayo makosa .

Source:Millard Ayo

Thursday, July 25, 2013

JOKATE, MUSSA KIPANYA WAZUA JAMBO



Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ katika pozi na Mtangazaji Mussa. 
MWANAMITINDO na mtangazaji maarufu Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Mtangazaji Mussa wa runinga wamezua jambo kufuatia picha zinazodhihirisha urafiki wao uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi kunaswa.
 
 Awali paparazi wetu aliinasa picha ya wawili hao ambayo kwa mujibu wao, walipiga miaka kumi iliyopita na walipokutana tena mwaka huu wakapiga mpya.
Baadhi ya wadau walioziona kwa mara ya kwanza, waliibua minong’ono kuwa urafiki wao ni wa siku nyingi hivyo kuna uwezekano wakafikia hatua ya ndoa.
“Urafiki wao ni wa kitambo, wanaweza kuja kuoana kabisa sababu aina ya maisha yao ni ya usiri sana,” alisema mdau mmoja ingawa wenyewe wamesema hawana cha kuzungumza juu ya hilo

Musa na Jokate katika picha ambayo inadaiwa kupigwa miaka kumi iliyopita. .

PENZI LA FEZA KESSY NA ONEAL LAZIDI KUPAMBA MOTO KWENYE JUMBA LA BBA.....FEZA KESSY AKIRI KUFA KIMAHABA


“We’re getting more serious,” Feza alimwambia Big Brother. “Kukutana na Oneal kwenye nyumba hii kumeonesha upande wangu ambao sikudhani watu wangeuona, alisema Feza. Upande wa ulaini na udhaifu wangu. Marafiki zangu nyumbani wanasema nimekuwa rahisi sana na napotea. Mtu mmoja anahitaji kwa kiasi fulani kuwa mjinga kwenye uhusiano. Ni ngumu sana pia, sababu wakati mwingine nataka kuwa mkali na siwezi sababu uhusiano huu si tu unanihusu mimi. Unanihusu mimi Oneal na Africa.” Feza alimwambia Biggie kuwa yeye na mpenzi wake huyo raia wa Botswana wana hamu kubwa siku wanaondoka mjengoni humo kwenda kuundeleza zaidi uhusiano wao.

WEMA SEPETU ANUNUA GARI JIPYA LA PINK



Wema Sepetu amenunua gari jipya la rangi ya pink kutokana na maneno ya meneja wake Martin Kadinda aliyoandika facebook na kuweka picha ya Wema akiwa na gari hilo "
samahani kwa ubora wa picha kuwa hafifu....... Ila huyu dada anapenda pink kupitiliza..... haya she gat new pink Car.... mkutane barabarani..." aliandika Martin. Licha ya gari hilo kutotajwa gharama yake wema ni kati ya mastar wa kike wanaomiliki magari meng kwa sasa yakiwemo pia ya gharama kubwa anayomiliki Movie star huyo

BAADA YA KUPIGWA CHINI BIG BROTHER, HUDDAH AAMUA KUMALIZA HASIRA ZAKE KWA KUJIPIGA UCHI



Wengi waliamini kwamba Big Brother imempa fundisho mrembo huyu na kutegemea mabadiliko makubwa ikiwa ni pamoja na kuuuheshimu mwili wake baada ya Video zake za uchi kuvuja akioga bafuni...
Hali imekuwa ni tofauti kwa mrembo huyu asiyeijua thamani ya mwili wake.Tabia ni ngozi.Skendo,picha za uchi huenda ziko katika mishipa ya damu yake....

Hizi ni picha zake za nusu uchi alizotupia mtandaoni.


Wednesday, July 24, 2013

RAY C NA RECHO KUFANYA BONGE LA KOLABO


Mwanamuziki wa kitambo Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ana matarajio ya kurudi katika game baada ya kuwa fiti sasa kiafya. Kupitia mtandao wa instragram Ray C amekuwa akitupia picha zinazomuonyesha akiwa na afya nzuri tena kanona si haba!

Watu wengi wamekuwa wakimuhoji kupitia mtandao huo kuhusiana na mwanamuziki Recho kutumia style inayofanana na Ray C kama anafurahia au lah huku kukiwa na nmafikirio huenda hapendezwi na kitu hicho lakini ukweli ni kuwa Ray C anamfurahia na hivi karibuni wanarajia kudondosha kolabo kwa mujibu wa alichokiandika Instagram.
Alianza kwa kupost picha ya Recho..

Kisha akaandika maelezo..


Katika interview kadhaa Recho ameshawahi kukiri kuwa alivutiwa na Ray C kuingia katika muziki na ni mmoja katika ya wanamuziki anaowazimia mpaka leo na ndio maana style zao za uimbaji na uchezaji zinafanana.Ray C pia aliwahi kuandika ujumbe wa kuwashukuru mashabiki wake kwa kumsapoti alipopata matatizo ya kiafya mpaka leo.
Najaribu kuvuta picha ya kolabo ya wawili hawa halafu siipati hiyo picha yenyewe

VAZI LA NUSU UCHI LAZUIA NDOA KUFUNGWA JIJINI DAR....PADRI AGEUKA MBOGO NA KUWATIMUA WAPAMBE



KIVAZI cha ndugu wa maharusi, kimesababisha patashika katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Peter, baada ya Paroko Msaidizi wa Kanisa hilo, Padri Paulo Haule, kusitisha ibada mpaka mhusika atoke akavae vizuri.

“Ninatoa dakika 10 kwa aliyeingia na mavazi ambayo hayatakiwi kanisani humu kutoka mara moja akavae vizuri, la sivyo ndoa yao haitafungwa,” alisema Padri Haule wa Kanisa hilo lililoko Oysterbay, Dar es Salaam.

Awali vurugu hizo zilizotokea Jumamosi iliyopita, zilianzia nje, wakati Katekista wa Parokia hiyo, Yohane Maboko, alipotangazia wanandoa na ndugu zao waliokuwa mabega wazi au kuvaa nguo fupi, kutafuta nguo za kujifunika au wasiingie kabisa kanisani.

Maharusi walikubali kutekeleza ombi hilo, wakavishwa vitambaa mabegani vya rangi tofauti na gauni jeupe la harusi, wakaruhusiwa kuingia kanisani, tayari kufunga pingu zao za maisha.

Hata hivyo, mmoja wa ndugu wa maharusi hao ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alipotaka kulazimisha kuingia na kivazi chake cha mabega wazi, alizuiwa na Katekista Maboko. Katekista huyo alimfuata mwanamke huyo ili kumrudisha akavae vizuri, lakini aliibua zogo na kulazimisha kuingia na vazi hilo.

Zogo hilo lilipoendelea, wanandugu waliingilia kati, wakitetea vazi hilo ambapo mmoja wa wanandugu, alimvua miwani Katekista Maboko na kuipiga chini ikavunjika huku yeye na wenzake wakimtolea maneno makali ya kumtaka asimzuie ndugu yao kuingia kanisani.

Wakati ndugu hao wakimdhibiti Katekista Maboko, mwanamke huyo alitumia mwanya huo na kupenya hadi ndani ya Kanisa, ambamo Padri Haule, alikuwa akijiandaa kuanza ibada.


Baada ya Padri Haule kupata taarifa, alitangaza kuwa ndoa ya maharusi wa msichana huyo, haitafungwa hadi awe ametoka.

Licha ya Paroko kutangaza hivyo, bado ukaidi uliendelea jambo lililomfanya Katekista Maboko kumfuata tena dada huyo na kumwamuru atoke nje, ambapo aliendelea kupinga na baadaye akatekeleza amri hiyo ya Paroko.

Baada ya hapo shughuli za kufungisha ndoa ziliendelea kwa amani na utulivu hadi mwisho maharusi wakatoka kwenda kuendelea na mambo mengine.


Akizungumza na mwandishi wetu, Katekista Maboko alisema waumini hao walikiuka maadili ambayo Kanisa lina wajibu wa kulinda na kuyasimamia ili waumini wake wayafuate.


Alisema miwani yake iliyovunjwa ilikuwa na thamani ya Sh 90,000 na baada ya ibada hiyo, aliyetenda kosa hilo alimwendea na kumwomba radhi na kulipa Sh 50,000 na kuahidi kumalizia kiasi kilichobaki wakati wowote.

Maboko alisema uvaaji wa mavazi yasiyotakiwa kanisani hapo, umekuwa ukipigiwa kelele mara kwa mara, na hata katika mafundisho ya ndoa huambiwa lakini ukaidi unaendelea.


“Maharusi wakati wa mafundisho ya ndoa tunawaambia kuhusu mavazi yao na hata ya ndugu zao watakaowasindikiza kanisani, kuwa wavae kistaarabu lakini hawasikii,” alisema Katekista Maboko.
Makanisa mengi siku hizi yamekuwa yakipiga marufuku uvaaji wa nguo fupi na zinazoacha mabega wazi kwa wasichana na wanawake, wakati wa ibada za kawaida na za ndoa.

IRENE UWOYA NA LUCY KOMBA WASHIKANA UGONI



NYOTA wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krrish’ ametoa kali ya mwaka baada ya kudai kwamba amemshika ugoni msanii mwenzake, Lucy Komba mara baada ya kuziona picha za msanii huyo akiwa na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ wakiigiza filamu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutokea nchini Swaziland, Uwoya amepinga vikali utetezi unaosemwa kwamba Lucy na Kataut walikuwa wakishuti filamu na anaamini kuwa msanii huyo ameamua kumzunguka na kutaka kuibomoa ndoa yake.

“Lazima kuna kitu kinaendelea kwani katika dunia hii sijawahi kuona filamu inayochezwa na watu wawili tu mwanzo mpaka mwisho, ninachotaka kusema ni kwamba Lucy ana mpango wa kuiharibu ndoa yangu,” alisema Uwoya kwa hasira.



Uwoya amehoji usiri wa filamu hiyo na kila alipokuwa akimpigia simu mumewe alikuwa akimjibu kwamba yuko Rwanda kumbe alikuwa Bongo akiigiza filamu na Lucy.

“Kwanza Lucy ashukuru niko mbali, laiti ningekuwa karibu angenieleza vizuri kwa sababu hata yeye angeweza kunipigia simu na kunifahamisha ushiriki wa mume wangu kwenye filamu hiyo kwa kuwa namba zangu anazo, ilikuwaje hakufanya hivyo?” alihoji.

Kuonesha kwamba amechukizwa na kitendo hicho, Uwoya alisema kwamba akitua Bongo atamtafuta Lucy ili aweze kumshughulikia vizuri na ikiwezekana amuoneshe hiyo filamu waliyoigiza watu wawili tu.

“Nitatua Bongo siku si nyingi na cha kwanza ni kumtafuta Lucy, anieleze vizuri kuhusu filamu hiyo waliyocheza na mume wangu,” alisema Uwoya.

Filamu hiyo ambayo imekuwa maumivu makubwa kwa Uwoya, imechezwa na Lucy na Ndikumana tu mwanzo hadi mwisho na imepewa jina la Kwa Nini Nisikuoe.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...