Saturday, July 14, 2012

YOTE ALIYOSEMA MASANJA MKANDAMIZAJI KUHUSU KUWA MCHUNGAJI.



Cover ya album ya gospel ya Masanja Mkandamizaji.

Japo wengi wamezoea kumuona akichekesha kwenye Orijino Komedi ya TBC 1, kuna kitu kingine inawezekana haujakifahamu kuhusu Masanja, ni kwamba ni yeye ni Mchungaji Mtarajiwa.

Amesema ” mimi ni mchungaji mtarajiwa na hii sio nataka, hii ni vile maono tu jinsi Mungu amesema na mimi unajua swala la uchungaji sio la wewe unataka, hapana……ni vile Mungu amesema nini na wewe, sasa kasema na mimi niwe Mchungaji kwa hiyo mimi ni Mchungaji mtarajiwa usiulize lini wala saa ngapi, wakati wowote wa bwana utakapofika mwanawane”


“Kwa mfano hapa Dar es salaam kila jumamosi, jumatano na ijumaa kanisa letu linafanya ibada za mitaani utakuta lifuso linapita barabarani limeandikwa Miito ya Baraka unanikuta mtumishi wa Mungu nimekamata mic tunahubiri injili na watu wanaokoka kwa hiyo vile mi sijali hata mtu akisema nachekesha, we ona nachekesha lakini kwenye ufalme wa Mungu inahesabika watu wengi waliokoka baada ya kuhubiriwa na Masanja sasa mimi nina shida gani” – Masanja

Kuhusu kuacha kazi ya Uchekeshaji na kujiweka kwenye kazi ya Mungu zaidi, Masanja amesema “ikitokea Mungu akasema na mimi kwamba hii stopisha sasa twende na kondoo wa bwana nitafanya hivyo lakini kwa sasa pia vyote vyote tu, komedi inaendelea” Masanja Mkandamizaji jumapili ya July 15 2012 Iringa 92.9 ataitambulisha album yake ya Gospel kwenye uwanja wa Samora ikiwa ni album iliyoandaliwa kwa miaka miwili na miezi saba, siku ya unzinduzi ataungwa mkono na Faraja Mtaboba, Martha Mwaipaja na wengine
Habari/picha:Milard Ayo blog

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...