Thursday, July 12, 2012

MREMBO BORA WA MISS SINZA 2012 KUPATIKANA KESHO, TWANGA KUWASHA MOTO

Mwalimu wa warembo wa shindano la kumsaka Miss Sinza 2012, Mwajabu Juma, akitoa maelekezo kwa warembo hao wakati wa mazoezi yao ya mwisho kujiandaa na shindano hilo litakalofanyika kesho katika Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hoteli, Sinza. Shindano hilo litasindikizwa na burudani kabambe na shoo ya kufa mtu kutoka kwa Bendi ya African Stars, watakaokuwa wakitambulisha pia baadhi ya nyimbo zao mpya kwa mara ya kwanza, pamoja na msanii wa Vichekesho kutoka kundi la Ze Commedy linalorusha michezo yake kupitia Televisheni ya Chanel 5, Masawe Mtata, ambaye pia atakuwa akitambulisha video ya wimbo wake mpya uitwao Uongo Kweli. 
 
Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 14 wanaowania taji la kituo hicho pamoja na kuiwakilisha kitongoji cha Sinza kwenye mashindano ya Kanda ya Kinondoni na baadaye Miss Tanzania.
Mbali ya taji (crown) na nafasi ya kuiwakilisha Sinza katika Mashindano ya Kanda ya Kinondoni, pia mshindi wa kwanza katika shindano hilo atajinyakulia kitita cha sh. 500,000/= katika mashindano hayo yatakayopambwa na bendi ya African Stars “Twanga Pepeta International’ ambao watakuwa wakitambulisha baadhi ya nyimbo zao mpya na Msanii wa vichekesho wa kundi la Ze Comedy la Chanel 5, Masawe Mtata, atakayekuwa akitambulisha video na wimbo wake mpya wa Uongo Kweli.
Akizungumza na mtandao huu, Mratibu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Calapy Entertainment, Majuto Omary, alizitaja zawadi nyingine kuwa ni shs 400,000 kwa mshindi wa pili, sh. 300,000 kwa mshindi wa tatu . Mshindi wa nne na wa tano watapata sh. 150,000 kila mmoja na waliobaki watapata sh. 100,000 kila mmoja kama kifuta jasho.
Aidha Majuto, aliongeza kuwa mbali ya kutembea jukwaani kwa ‘catwalk’ kwa warembo hao, pia kutakuwa na shindano la kusaka vipaji ambapo warembo watachuana ili kumpata Mafoto Miss Talent Sinza 2012, ambapo mshindi atapata sh. 50,000 kutoka mtandao wa sufianimafoto.blogspot.com.
“Maandalizi yamekamilika na viingilio vitakuwa ni sh. 10,000 kwa viti vya kawaida na sh. 25,000 kwa vitu Maalum (VIP), tumeandaa shoo fupi na ya aina yake ili baadaye mashabiki wa fani ya urembo wa kitongoji cha Sinza wapate fursa ya kusugua kisigino na bendi ya Twanga Pepeta,” alisema Majuto.
Majuto aliwataja Warembo wanaowania taji hilo kuwa ni pamoja na Mariam Miraji, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Judith Sangu, Eva Mushi, Vailet John na Esther Mussa.
Warembo wengine ni Christina Samwel, Nahma Said, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi, Brigitter Alfred na Merina Mushi.
Shindano hilo limedhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Gland Villa Hotel, Clouds FM, mtandao wa sufianimafoto.blogspot.com, Brake Point, Fredito Entertainment, Screen Masters, Lady Pepeta na flexi.

Warembo hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hotel.


Warembo hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hotel.

Warembo hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hotel.

Warembo hao wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kumaliza mazoezi yao.

Warembo hao wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kumaliza mazoezi yao.
MASHINDANO ya kumsaka mrembo bora waKitongoji cha Sinza, Redds Miss Sinza 2012 yatafanyika kesho (Ijumaa) kwenye ukumbi wa Mawela Social Hall (Ten Star Lounge) uliopo karibu na hoteli ya Vatican City.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...