Thursday, July 12, 2012



.

Baraza la Habari la Kiislamu Tanzania BAHAKITA limesema linakusudia kuwafungulia mashitaka madaktari bingwa wote na madaktari waliokuwepo kwenye mafunzo kwa vitendo ambao walishiriki katika mgomo kwenye hospitali mbalimbali nchini na kusababisha wagonjwa kukosa huduma za matibabu huku wengine wakipoteza maisha yao.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya baraza hilo kukaa na madaktari waliokua katika mgomo na kukubaliana kuwa waiombe radhi serikali pamoja na wananchi warudi kazini lakini madaktari hao wamekiuka makubaliano hayo na kuendelea na mgomo jambo lililoonyesha kwamba hawakuwa tayari kupata suluhu.

Katibu wa BAHAKITA Said Mwaipopo amesema wameshauriana na wanasheria wao na kuamua kuwafungulia kesi ya mauaji Madaktari hao katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es salaam july 16 mwaka huu.

Amesema “kwa tukio zima jinsi lilivyokwenda limeonyesha kwamba madaktari hawataki wala hawana shida tena ya kurudi kazini kwa sababu ni wazi kwamba kuna mtu yuko nyuma yao wanaemtumikia, sisi kama Watanzania sehemu ya jamii tumekaa na wataalamu wetu wa sheria tumekubaliana kwamba jumatatu tunakwenda kufungua kesi Mahakamani kwa Madaktari wote waliogoma wakati wamesomeshwa na kodi zetu na serikali yetu imewasomesha, tutawafungulia kesi ya kusababisha mauaji pale Muhimbili kwa hiyo tunachofanya hivi sasa ni kwenda pale Muhimbili kwa mganga mkuu kuchukua orodha ya watu waliopoteza maisha”

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...