Wednesday, January 4, 2012

UZINDUZI DAR LIVE NI HISTORI YA MWAKA 2012

Juzi niliuanza mwaka kwa kuhudhuria uzinduzi wa kiota kipya na cha aina yake kilichopo maeneo ya Mbagala Zakheim jijini Dar-es-salaam. Mwanzoni nilipoambiwa kwamba kuna kitu cha aina yake kinazinduliwa maeneo ya huko nilidhani ni kitu cha kawaida tu yaani ukumbi mwingine wa ziada kati ya kumbi nyingi zilizopo.Nilikuwa nafanya makosa kwani baada ya kuona nilichokiona,naomba nikiri kwamba Dar Live ni mojawapo ya kumbi za kisasa kabisa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.Ni mahali ambapo familia nzima inaweza kupata mapumziko na burudani za kutosha.Kuna sehemu nyingi kwa michezo ya watoto,counter za kutosha kwa vinywaji,nyama choma na jukwaa la kisasa lenye lighting safi.

Kingine ambacho nilikuwa sijakipigia hesabu vizuri ni idadi ya watu.Kama sote tunakubaliana kwamba shughuli ni watu,basi ule uzinduzi wa Dar Live ulifana kwa style ya aina yake kabisa.Hongera sana kwa wadau wote wa Global Publishers kwa uzinduzi safi na eneo safi.Hizi hapa ni baadhi ya picha kutoka katika uzinduzi huo


Professor Jay “akiwabatiza” mashabiki waliohudhuria uzinduzi wa Dar Live


Gangwe Mob wakifanya vitu vyao katika uzinduzi huo.




DJ Ommy & One B ambao waliongoza shughuli hiyo jukwaani.




Juma Kassimu a.k.a Sir Nature akitoa burudani.




Mzee Yusuph kutoka Jahazi Modern Taarab akifanya vitu vyake.




Sehemu ya umati ya mashabiki waliohudhuria.




Sehemu ya raha ya watoto




Professor Jay sambamba na mdogo wake,Kolihombi,jukwaani




Gangwe Mob wakiwa kibaruani.




Wanaume wakiwa kazini



No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...