Saturday, January 7, 2012



washiriki wa BBA mwaka jana. 
Siku sita baada ya mwaka mpya kuanza, M-NET imetangaza rasmi kuhusu shindano ambalo mwaka huu linatimiza mwaka wa saba, BIG BROTHER AFRICA. afisa uhusiano wa MULTICHOICE TANZANIA Barbara Kambogi amesema BBA ya mwaka huu itaanza mapema MAY, na itakua tofauti kuliko season nyingine zote zilizotangulia, ambapo bado mpaka sasa hivi haijajulikana jinsi washiriki watakavyochaguliwa lakini details nyingine zinakuja. Big brother ya mwaka jana ilianza mwezi huo huo wa may, ambapo wiki mbili baadae, Mtanzania Lotus ndio alikua mshiriki wa kwanza kutolewa kwenye jumba la BBA baada ya kuvunja masharti kwa kumpiga Lucle wa Afrika kusini ambapo baada ya kutolewa, alisema adhabu aliyopewa ilikua kubwa kwake kuliko ya Lucle ambae alipewa kazi ya kuosha vyombo tu.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...